Viongozi wa klabu na mabaraza ya watoto kutoka Halmashauri tatu za Mkoa wa Arusha,  Meru, Karatu na Jiji wakiambatana  na  viongozi toka Ofisi  ya  Rais TAMISEMI, Wataalamu  wa  Mkoa wa Arusha  na Halmashauri  pamoja na Viongozi na watumishi toka Shirika la  SOS CHILDREN'S  VILLAGE wamepata fursa ya kufuatilia shughuli  za  Bunge la Jamhuri  ya  Muungano  wa Tanzania leo tarehe 13/06/2023 ikiwa ni sehemu ya ziara ya mafunzo ya siku tano jijini Dodoma. 

Viongozi hao wa klabu za Watoto wameshuhudia namna muhimili wa Bunge unavyoendesha shughuli zake ambapo pia watapata fursa ya  kutembelea chuo  cha Dodoma, Mji wa  serikali mtumba na kushiriki maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika ambayo inahitimishwa Kitaifa Mkoani Dodoma  tarehe 16/06/2023. 

Hilda Mgomapayo  kutoka Ofisi ya Rais  TAMISEMI, ambaye ni mratibu wa dawati la ulinzi, usalama na maendeleo ya mtoto amesema Serikali  kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI  inasimamia  na kuratibu uundwaji wa Klabu hizi ikiwa ni utekelezaji wa  sera ya Mtoto,Sheria  za Nchi na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa. 

Ikumbukwe  shirika la SOS CHILDREN'S VILLAGE Kwa kushirikiana na Serikali kupitia Mkoa wa Arusha na Halmashauri waliwezesha kuundwa Kwa klabu za watoto mashuleni ambazo zimekuwa msaada na jukwaa muhimu la kuwasilikiliza watoto lakini pia kupokea changamoto zao na kuzifanyia kazi.

Awali akizungumzia umuhimu wa ziara hiyo , Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Arusha ndugu Denis Mgiye amesema Watoto  watapata uzoefu na kuongezewa ujasiri wa namna ya kuendesha vikao vyao na kuibua masuala mbali mbali yanayohusu ulinzi na usalama wa Mtoto.

Naye, Afisa Maendeleo ya jamii anayeratibu na kusimamia uundwaji na uendeshaji wa klabu za watoto Mkoa wa Arusha

Bi.Erena Materu amehimiza uundaji  wa klabu hizo katika shule zote na ngazi ya jamii  kunawasaidia watoto kujisemea na kuomba ushirikiano zaidi,kupewe umuhimu  kutoka Idara za kisekta na wadau mbali mbali.






Share To:

Post A Comment: