Na Tumaini Mafie,Arusha


VIJANA wa vyuo vya Sanaa nchini waiomba Serikali kutoa sapoti kwa wasanii Ili kuweza kufanya kazi Yao Kwa upana zaidi Kwa lengo la kuelimisha Jamii kupitia kazi zao.

Walitoa rai hiyo mkoani Arusha wakati walipokutana Kwa ajili ya kuonyesha vipaji vyao na kutembelea Jamii ikiwemo makundi maalumu Kwa ajili ya kuhamasisha Jamii kupitia kazi za Sanaa.

Wakizungumza Kwa nyakati tofauti vijana hao walisema Sanaa inaleta mabadiliko chanya Kwa Jamii na ina uwezo wa kuingiza Pato la Taifa pale inapothaminiwa.

Nkosi Nathi kutoka Washington Marekani alisema Sanaa imekuwa ikisahaulika na Serikali hazitoi vipaumbele kwa wasanii hivyo soko lake Kutokukua na wasanii kukata tamaa.

"Hatupewi vitendea kazi mfano kupatiwa studio za kisasa kufanyia kazi zetu kutoka Kwa Serikali zetu, lakini pia tukikumbuka Sanaa inaleta watu pamoja hivyo Serikali iangalie kazi za wasanii na kuzithamini"alisema Nathi.

Jasmine Smalls kutoka Marekani alisema Sanaa inaweza kuongeza Pato la Taifa pale inapothaminiwa na kupewa sapoti na Serikali.

"Unatumia nguvu kubwa katika kujipatia Elimu ya Sanaa na kutumia pesa nyingi katika kujenga kipaji hivyo ni wakati muhimu sana pale unapokuwa umehitimu upate pakufanyia hiyo Sanaa Yako na upate kipato kupitia Sana yenyewe " alisema Smalls.

Dk. Romita Sillitti  alisema kupitia vipaji Jamii inaungana pamoja na kujengwa kisaikolojia na pia kupitia vipaji watu hutoka sehemu moja kwenda nyingine Kwa lengo la kujifunza na kuonyesha vile walivyonavyo.

Nathi Mncube ni msanii kutoka Marekani naye alisema Sanaa inajenga na kupitia Sanaa amepata nafasi ya kuzunguka nchi Mbalimbali  na kuelimisha kupitia kipaji chake na hivyo alisema anavutiwa zaidi na kazi ya Sanaa na kuahidi kuiendeleza.

Aidha katika tamasha hilo la Sanaa liliwakitanisha vijana kutoka vyuo Mbalimbali hapa nchini ikiwemo TAI  Cha mkoani Mbeya kinachotoa mafunzo ya Utamaduni, Sheroes, Kituo Cha Sanaa, Rungwe College of Business, TASUBA  Bagamoyo na Chuo Cha Dar Es salaam.

Share To:

Post A Comment: