Na John Walter-Mbulu

Hospitali ya Kilutheri Haydom Dayosisi ya Mbulu imeandaa mbio za nyika (HAYDOM MARATHON 2023) kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wasioweza kugharamia matibabu hospitalini hapo na kuboresha huduma zaidi.

Mkurugenzi wa Hospitali hiyo Dr.Pascal Mdoe akizungumza na waandishi wa Habari, amesema  kupitia mbizo hizo wanakusanya fedha kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kulipia matibabu ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kukusanya zaidi ya shilingi Milioni 100.

Mbio hizo zinafanyika mara ya sita mfululizo ambapo kwa sasa itakuwa Mei 27,2023 katika kata ya Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara na kushirikisha wakimbiaji wa ndani na nje ya nchi.

Aidha Dr. Mdoe amesema bei za matibabu katika hospitali ya Haydom ni nafuu akitolea mfano, “mama kujifungua mtoto ni shilingi elfu 25,000 pekee na nguo za kuanzia kwa mtoto”

Aidha amewataka wadau ambao wapo tayari kuchangia zaidi ili kuwasaidia wananchi hao.

Katibu wa kamati ya maandalizi Haydom Marathon 2023 Dr. Rose Raphael amesema mbio zinatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 1,000 na pia zinafanyika katika maeneo mbalimbali hata nje ya nchi kama marekani na Norway kuunga mkono jitihada hizo.

Mwenyekiti wa kamatai ya maandalizi ya Mbio hizo za Nyika Haydom Marathon 2023 Joseph Nicodemus amesema mbio zitakazokuwepo ni kilomita 21, kilomita 10,na kilomita 2 za kujifurahisha huku zawadi zikitolewa kwa washindi ambapo zaidi ya shilingi milioni tano kushindaniwa.

Wananchi wote  wanakaribishwa  kushiriki mbio hizo kwa kujiandikisha kwa shilingi elfu 25,000 pekee ambapo utapatiwa t-shirt na medali, Mei 27,2023 kuanzia saa 12:00 asubuhi.

 

 

 

Share To:

Post A Comment: