Chuo cha uhasibu Arusha (IAA)kimewataka wanafunzi  mbalimbali wanaosoma katika chuo cha Uhasibu Arusha kukitumia kituo cha kiatamizi kwa ajili ya kuendeleza bunifu zao na kuweza kufikia malengo yao.

Hayo yalisemwa  jijini Arusha na Profesa Eliamani Sedoyeka  wakati akizungumza katika maonesho ya mafunzo ya ufundi Stadi  yanayofanyika katika viwanja  vya Stadium  jijini Arusha.

Profesa Sedoyeka amesema kuwa,kituo hicho kimeweza kuwasaidia vijana waliohitimu chuoni hapo kwa kuweza kuanzisha biashara zao mbalimbali na kuweza kujiajiri na hata kuajiri wengine.

Amesema kuwa ,kituo hicho kina malengo mbalimbali ya kuwatafutia mitaji,kuboresha uzalishaji,kuwasaidia kupata masoko ya uhakika na hatimaye kufikia kampuni.

Ameongeza kuwa,kitendo cha kuwaandaa vijana wao kinawasaidia wao kuweza kujiajiri na kuajiri wengine huku kampuni zao zikizidi kukua na kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni kuunga mkono lengo la kujenga Tanzania ya viwanda ambapo kituo kimejipanga kukuza zaidi ya biashara 40 kwa wakati mmoja.

Amefafanua kuwa,vijana  wenye wazo la biashara wameweza kuwasaidia kuwa wazo la makampuni ambapo kwa mwaka huu wamewawezesha vijana hao kuanzisha makampuni 6 .

Aidha ameongeza kuwa,kwa mwaka huu chuo hicho kimeweza  kuanzisha kozi mpya ya bachelor  degree ambayo imewezesha  kuzalisha wataalamu wa kutosha ,ambapo amewataka vijana waliohitimu  kidato cha sita ndio  muda wa kuchangamkia  fursa hiyo kwa kujifunza kozi  mbalimbali chuoni hapo. 

"Sisi tumejipanga kwa kutoa kozi za kimkakati  ikiwemo ya uanagenzi  katika maswala ya bima,na utalii ambapo wanafunzi wetu wamekuwa wakiandaliwa  vizuri na kupata muda  mzuri  wa kujifunza zaidi."amesema Profesa Sedoyeka.












Share To:

Post A Comment: