Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 


Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Wilaya ya Chemba Said Sambala ametoa wito kwa madiwani wa Halmashauri hiyo kutumia vizuri fedha zinazotolewa na Serikali katika kutekeleza miradi ya Maendeleo ikiwa ni pamoja na mradi mkubwa wa Shule mpya ya Busi.

Mheshimiwa Sambala ametoa wito huo leo Mei 17, 2023 wakati akifungua kikao Cha baraza la madiwani Robo ya tatu huku akisema miradi hiyo ikisimamiwa vizuri Serikali itaedelea kutoa fedha kwaajili Halmashauri ya Chemba.

"Tuhakikishe tunasimamia vizuri hii Miradi ili thamani ya fedha ionekane na wananchi waendelee kukiamini Chama Cha Mapinduzi CCM".Ametoa wito Sambala

Ameongeza kwa kutoa rai kwa madiwani hao kutoa elimu ya tahadhari kwa wananchi kutunza chakula na hata katika usimamizi wa Mapato ya Halmashauri kwa wale wanaouza Mazao yao kutokana na Neema ya Mvua zilizonyesha kwani kuna uwezekano wa Kuvuna Mazao kwa wingi pamoja na changamoto za kuvamiwa na Wanyama Wakiwemo Tembo na Nyati .


"Pamoja na changamoto za wanyama mbalimbali ikiwemo Tembo na Nyati ambao wanavamia Mashamba lakini mategemeo nikwamba tutavuna angalau hivyo kwa wale wanaouza Mazao sisi tuongeze umakini katika usimamizi hasa katika eneo la kukusanya  mapato".Amesema

 Na Kuongeza " ifike mahala tukubaliane kwenda katika njia sahihi ili tuweze kwenda kwenye Miongozo na maelekezo yote ya Serikali namna ya kuendesha Mamlaka ya  Serikali za mitaa, Naamini tukifanya hivyo tutatimiza malengo yetu tuliyojiwekea na Chama kitakua kimetimiza Malengo yake maana Chama ndiyo kimeunda Serikali". Ameongeza Sambala


Naye Kaimu Manager wa RUWASA Chemba Robert Maganga Amesema rai yake ni kwa Madiwani wa Halmashauri hiyo kushiriki kikamilifu Kwenye usimamizi wa miradi ya Maji inayoendelea kutekelezwa ili kuondoa changamoto ya kutokamika miradi hiyo kwa wakati na Kuleta kero kwa wananchi.

" Tunayo miradi inayotekelezwa na tukishirikiana tukawa kitu kimoja tutakua tumeondoa changamoto ya kusuasua kwa miradi hii na hata kutokamilika kwa wakati hivyo tuwatoe hofu wananchi kwamba kazi inaendelea".Amesema Maganga

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Abdi Msuri ambaye pia ni Diwani katana ya Jangalo Amesema katika kikao hicho jambo kubwa lililojadiliwa ni usimamizi wa fedha zinazotolewa na Serikali ili thamani ya fedha hizo zilingane na shughuli husika ikiwa darasa basi ilingane na thamani ya fedha zilizotolewa.

"Pia tumezungumza  suala la ukusanyaji wa Mapato kwamba lazima tusimamie Mapato kwasababu Mapato ndiyo roho ya kuiendesha Halmashauri". Amesema Msuri

Aidha Amesema kimsingi Mtendaji wa Kijiji anatakiwa akae kwenye kituo chake cha kazi lakini kwa kikao kilichofanyika kata ya Chandama kilichoitishwa na katibu wa Chama Cha Mapinduzi imeonekana watendaji wengi sana wanakaa nje ya vituo vyao vya kazi  jambo ambalo linawagarimu wananchi kumfata huko alipo.

"Na Mtendaji wa kata / Kijiji ni kama Polisi pale yapo matukio ambayo yanatokea usiku inatokea mwananchi anatoka kilomita 30 usiku anamfuata Mtendaji wakati Sheria inamruhusu yeye akae eneo la kituo cha kazi kwa hiyo tumeomba Afisa Utumishi awaandikie Watendaji wote barua wale ambao wanakaa nje ya Vituo warudi wakae ndani ya Vituo vyao vya kazi". Amesisitiza Msuri

Alhaji Shaban Kilalo ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Chemba amesema Madiwani ni watendaji wanaotegemewa na Chama hivyo wanapaswa kusimamia vizuri Fedha zinazotolewa na Mheshimiwa  Samia Suluh Hasan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: