Ndivyo unavyoweza kusema baada ya TFS kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Shule Kuu ya Sayansi ya Akua na Uvuvi (SoAF) kufanya utafiti katika Bwawa la Minaki lililopo katika Hifadhi ya Pugu. Utafiti huu umefanywa na jumla ya wataalam 8 ambao umelenga katika kujua taarifa za kina kuhusu Bwawa hilo ambalo pia ni mojawapo ya kivutio cha utalii katika Hifadhi hiyo. 

Utafiti unataka kujua hali halisi ya Bwawa kuanzia urefu wa kina, ukubwa, viumbe wanaoishi ndani ya maji, hali ya udongo chini ya maji, mimea kando na ndani ya Bwawa, wadudu wanaoweza kusababisha magonjwa na hali ya chakula kwa viumbe hasa samaki wanaopatikana katika Bwawa hilo. 

Utafiti huu umefanyika baada ya serikali kuona ipo haja ya kutafuta taarifa za kina kuhusu kivutio hiki cha utalii na ili pia kujibu kiu ya muda mrefu waliyokuwa nayo watalii wanaotembelea Hifadhi waliokuwa wakionesha nia ya kutaka kuogelea ndani ya Bwawa. Utafiti huu pamoja na mengine utasaidia kupata majawabu sahihi ya nini kilichopo  na matumizi sahihi ya Bwawa la Minaki.

Timu ya wataalam 8 iliongozwa na Dkt. Blandina Lugendo ambaye ni Mkuu wa Shule kuu ya Sayansi ya Akua na Uvuvi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

Matokeo ya utafiti huu yataisaidia serikali kupanua wigo wa matumizi ya Bwawa hili na kusaidia katika kuongeza thamani ya utalii ikolojia katika Hifadhi ya Pugu.

Share To:

Post A Comment: