Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 

Waziri wa Elimu, Sayansi, na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema  maoni yote yaliyotolewa katika Kongamano la wadau kuhusu Sera na Mitaala yatakwenda kuchakatwa.

Prof.Mkenda ameyasema hayo Leo Mei 14,2023,Jijini Dodoma wakati wa Kongamano lilioduma Kwa siku tatu tangu Mei 12-14 la kujadili Sera ya Elimu na Mafunzo kuhusu uhuishaji wa sera na Mitaala ya Elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center.

Kongamano la Sera na Mitaala ya Elimu kwa wadau limefungwa kwa kusikilizwa maoni ya kile kilichojadiliwa kwa muda wa siku tatu  Jijini Dodoma ambapo wajumbe mbalimbali waliweza kujadili na kutoa maoni yao miongoni mwake ni Elimu ya awali kuwa ni lazima pamoja na matumizi ya Tehama kutokana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.

Prof.Mkenda amesisitiza kuwa mafunzo ya amali yasiwe kwa ajili ya waliofeli, kutakuwa na shule za kilimo kwa mitaala mipya, pamoja na shule za michezo za serikali zitakazoanzishwa ili kulitekeleza hili.


Amesema kwa sasa wataanza na shule tisa zilizopo hawatafanya kwa kukurupuka bali hatua kwa hatua ili suala hili kubwa lifanikiwe.

"Katika Mafunzo ya Amali tunataka watu wasiyadharau kwani siyo kwa waliofeli tu bali kwa shule na Vyuo mbalimbali na kwa kuanza tunaanza na Vyuo 9 vya Veta kuanza kutoa mafunzo hayo".Amesema Mkenda 

Profesa Adolf Mkenda amesema kazi ya kukusanya maoni ya kuboresha mitaala na sera ya elimu inaendelea, watachakata maoni yote yaliyotolewa na wadau ili kupata kitu kizuri chenye tija kwa taifa.

“Suala kubwa kama hili hatuwezi kukurupuka. “Kazi ya kukusanya maoni inaendelea , tumesikiliza maoni mengi, na sisi tutaangalia na kufanyika kazi kwani kwenye sera kikitamkwa lazima tutekeleze,” amesema Prof. Mkenda 


“Kwenye sera ya elimu, mapitio ya sera ni sekta yote ya elimu inagusa kuanzia elimu ya awali hadi vyuo vya ualimu lakini katika mitaala tutagusa elimu ya awali msingi, sekondari, elimu ya ualimu, vyuo vya serikali na binafsi, huku kwenye elimu ya vyuo vikuu TCU ndio watakaoshughulika kupanga mitaala.

“Tuhakikishe tunapowafundisha watu VETA tukienda kwenye gereji tuwakute huko, kazi ya mitaala inaendelea na itakuwa endelevu siku zote, kazi tetu kubwa ni kujenga elimu ya kujitegemea,” amesema Prof. Mkenda 


Akifunga Kongamano hiyo,Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI Mhe.Deogratius Ndejembi amewataka wadau wote wa Elimu kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika safari waliyoianza ya maboresho ya Sera na Mitaala ya Elimu hapa nchini.


Amesema kazi inayofanywa na Wizara hiyo ni Kwa ajili ya maendeleo ya Taifa hivyo OR-TAMISEMI ipo tayari kutekeleza Sera zote zitakazotolewa ili kuchochea maendeleo ya Elimu Kwa ujumla.

"Nitoe Rai Kwa Wadau wote wa Sekta ya Elimu kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa Kwa Wizara ya Elimu katika kipindi Hiki Cha kupitia na kuboresha Sera na Mitaala kwani tukiwa na Sera madhubuti ya Elimu itapelekea hata wahitimu wetu kuwa Bora na kuweza kujiajiri na kuajirika Kwa urahisi Kwa wanakuwa wamepita katika misingi sahihi ya Elimu".Amesema Mhe.Ndejembi


Aidha,Mhe.Ndejembi amebainisha kuwa OR-TAMISEMI Kwa kuonesha umuhimu wa Mabadiliko haya ya Sera na Mitaala inakwenda kujenga Shule za Ufundi katika Halmaushiri zote ambazo hazijafikiwa na VETA.


"Ofisi ya RAIS TAMISEMI ni pacha wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kazi yetu kubwa ni kusimamia na kutekeleza Sera zinazotolewa katika Elimu maana sisi ni wamiliki wa shule zote za Serikali hivyo tuna wajibu mkubwa wa kuhakikisha Elimu inayotolewa ni Bora na Kwa kudhihirisha Hilo tunakwenda kujenga Shule za Ufundi Kila Halmashauri ambayo hakuna VETA na Mafunzo ya Amali yatatolewa pia huko vyeti vitatolewa ambavyo ni SAWA kabisa na vile vinavyotolewa VETA".Ameeleza


Kwa upande wake Katibu mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknologia Prof. Carolyne Nombo amewatoa hofu na kuwaahidi waliotoa maoni kwamba michango itaenda kuchakatwa upya na kuzingatiwa.Aidha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, utamaduni na Michezo
Prof. Kitila Mkumbo amesema utashi wa kiuongozi na ujasiri wa kusimamia mambo magumu ndio jambo linalopelekea utekelezaji kufanyika. 

Amempongeza Rais Samia kwa utashi na ujasiri wa kusukuma mambo magumu ikiwamo suala la sera na mitaala.

“Katika miaka mitano au 10 ijayo elimu yetu itakuwa imeimarika, niwatoe shaka elimu ina malengo makubwa mawili la kwanza ni kuwezesha kujua na pili ni elimu timizi".Amesema Prof. Kitila
Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: