Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson, akizungumza Leo Mei 18,2023 wakati alipotembelea na Kukagua Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) lililopo katika Maonesho yaliyoandalaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,kwa taasisi zilizopo Chini yake yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.


Na Okuly Julius-Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson amelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ,kwa kuendelea kubuni huduma zinazochochea maendeleo ya sekta ya Mawasiliano hapa nchini.


Amesema Shirika hilo limejipambanua katika utoaji wa huduma zake za Mawasiliano ambapo kwa sasa wameweza kufikisha huduma za Mawasiliano katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Dkt.Tulia ameyasema hayo Leo Mei 18,2023 wakati alipotembelea na Kukagua Banda la Shirika hilo lililopo katika Maonesho yaliyoandalaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,kwa taasisi zilizopo Chini yake yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.


Ambapo Mhe.Dkt.Tulia amesema kuwa TTCL imeifungua nchi kidijitali jambo ambalo limesaidia kuchochea maendeleo ya Mtu mmoja mmoja na taifa Kwa ujumla.


"TTCL wmeifungua nchi Kimawasiliano ukweli huo lazima tuusema Kwanza hili la kupeleka huduma ya Mawasiliano katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro ni jambo la kupongezwa Kwa nguvu zote Kwani sasa Kila mmoja anaweza kuwasiliana na ndugu na jamaa wakiwa hata huko huko kileleni haya ni maendeleo, "amesema Dkt.Tulia


Dkt.Tulia amezungumzia pia huduma zinazotolewa na Shirika hilo za Majumbani ikiwemo huduma ya Fiber Nyumbani Kwako na Smart home kuwa zinasaidia kurahisisha Mawasiliano na kusimamia ulinzi na Usalama.

Meneja wa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Jijini Dodoma Leyla Pongwe.

Meneja wa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Jijini Dodoma Leyla Pongwe, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Shirika hilo,amesema kuwa Kasi ya Shirika hilo katika kuleta mapinduzi ya Kimawasiliano ni kutaka kuhakikisha agenda ya Serikali inafanikiwa ya kutaka kufikia Uchumi wa Kidijitali ifikapo 2025.

"Serikali ina malengo ya kuhakikisha uchumi wa kidijitali unakuwa kwa kasi ifikapo 2025 sasa Jukumu letu kama Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL ni kufungua njia kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa,"amesema


Amesema TTCL imekuja na huduma Mpya yenye malengo ya kurahisisha upatikanaji wa huduma ya Mawasiliano na Usalama Kwa mtumiaji wa huduma hiyo.


Amesema kuwa katika kurahisisha Utalii Nchini wameweza kufikisha huduma ya Mawasiliano kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro hivyo Watalii wanaotembelea Mlima huo hawapati changamoto yeyote.


Ameongeza kuwa Shirika hilo lina huduma ya Fiber Mlangoni Kwako ni huduma anayopelekewa mtumiaji mpaka Nyumbani kwake Bure ambapo mtumiaji anachotakiwa kufanya ni kulipia kifurushi chake Cha Mwezi na kuendelea kutumia huduma ya Mawasiliano ya kimtandao bila changamoto yeyote.


"Ili kufikia Tanzania ya Uchumi ya Kidijitali ni lazima kuhakikisha kwanza huduma za mtandao ni Bora Kila mmoja awe na Mtandao wenye Kasi ndio maana tukaja na Fiber Nyumbani Kwako ili kuwawezesha watanzania kupata huduma hiyo,"amesema Bi.Leyla


Pia Bi.Leyla amesema ili kuhakikisha ulinzi na Usalama Majumbani Shirika hilo wamekuja na huduma ya Smart Home ambapo mtumiaji atakuwa ana uwezo wa kufuatilia mambo yote yanayoendelea Nyumbani kwake hata kama yeye hayupo Nyumbani kupitia Application hiyo inamuwezesha kujua Kila kitu kinachoendelea Nyumbani kwake.


Hivyo Mtumiaji akiwa na huduma ya Fiber Nyumbani Kwako na Smart Home anakuwa na uhakika wa Mawasiliano na Usalama wa Mali zake hata kama hayupo Nyumbani.


Pia amesema kuwa Kwa sasa Shirika hilo linajipanga kuhakikisha wanafikisha huduma ya Fiber katika nchi za jirani kupitia Mkongo wa Taifa ambao Kwa sasa huduma ya Mawasiliano imefika Kila Mpaka unaoizunguka Tanzania.


"Pia tuna Kituo Cha kuhifadhi Taarifa "DATA CENTER" Kituo hiki kinasaidia kuhifadhi taarifa na data za mtumiaji, mtoa huduma na hata taarifa za serikali zinaweza kuhifadhiwa kupitia Kituo hiki na zinakuwa salama kabisa hivyo niwakaribishe Kwaaji ya kuhifadhi taarifa zenu katika Kituo Chetu,"amesema Bi.Leyla



Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: