Na. Damian Kunambi, Njombe.


Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) limesema tayari limekwisha tangaza tenda kwa makampuni matano ya wachimbaji wadogo wa madini ya makaa ya mawe katika kata ya Nkomang'ombe wilayani Ludewa ambapo wachimbaji hao wanatakiwa kuwa na kiasi kisichopungua sh. Bl. 5.

Hayo ameyasema muwakilishi wa shirika la maendeleo Tanzania ( NDC) Florian Mramba alipokuwa katika mkutano na wananchi wa kata hiyo ambao wanaenda kupisha mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma ambao ulihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya mkoa na wilaya.

" Makampuni haya yakisha patikana yataanza kazi mara moja mara baada ya kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi hawa wanaoenda kupisha mradi ambao utafanyika hivi karibuni" Amesema Mramba.

Hata hivyo kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amewataka wananchi wanaoenda kupisha mradi huo  kutopaparika na fedha hizo na kuanza kujiingiza katika mambo ya anasa na kuwatia umasikini. 

"Pesa huwa zinakuja na mambo mengi yaliyo mazuri na mabaya hivyo wewe mwenyewe ndo utachagua upande wa kuelekea, najua hapa watapatikana wenye akili timamu na pia watapatikana walio wapumbavu". Amesema Mtaka.

Fidia hiyo ambayo ilisubiliwa kwa miaka mingi inaenda kunufaisha wananchi 650 katika kata hiyo ambapo serikali imekwisha toa kiasi cha sh. Bl. 5.2 kwaajili ya malipo ya wananchi hao.

Share To:

Post A Comment: