Umoja wa Wanawake Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi UWT   wamefanya ziara ya kutembelea Tarafa ya king'ori iliyopo Wilayani Arumeru Mkoani Arusha ili kutatua changamoto mbalimbali  wanazokutana nazo wakazi wa eneo hilo husani wanawake kukosa mikopo na ukatili wa kijinsia kwa watoto. 

Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha   Flora Zelothe na kugundua  changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa huduma bora ya Afya 

katika Zahanati ya kijiji cha Shishiton iliyopo Kata ya Maruvango kukosa  vifaa vya kutolea Huduma na kusababisha wakina mama kujifungulia majumbani. 

"Katika sekta ya afya kumekuwa na changamoto  kubwa  katika Zahanati  ya kijiji imekuwa na ukosefu wavifaa tiba ikiwemo vitanda vya kujifungulia wakina mama wajawazito, viti vya kukalia, dawa  na vitendea kazi  vingine  lakini tutajitahidi kulifanyia kazi jambo hili kwa wakati. " 

 Pamoja na changamoto ya afya vilevile ukosefu wa mikopo kwa wakina mama na vijana limekuwa tatizo kubwa ambapo Mwenyekiti wa UWT Mkoa amewataka  wanawake kukuza uchumi wa Taifa  kwa kujiunga kwenye vikundi vilivyo sajiliwa ili waweze kupata mikopo  inayotolewa na serikali kupitia Halmashauri.

Suala la ukatili wa kijinsia kwa watoto limekuwa likikuwa kwa kasi hivi sasa hivyo amewataka wakinamama kuwa  makini na  watoto kwenye  malezi kuwalinda  hususani watoto wakiume wamekuwa wakilawitiwa na kuketa madhara makubwa kiafya na kisaikolojia

"Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la ukatili wa kijinsia hususani ulawaiti kwa watoto  wa kiume hivi sasa watoto hawana usalama wakienda shuleni wanafanyiwa ulawiti,wakirudi nyumbani pia awana usalama hivyo wakinamama tuwe makini sana katika kuwalinda watoto  wetu"

Pia amewataka wananchi wa wilayani Arumeru kuchukua kadi za uanachama ili ziweze kuwasaidia kupata mkopo wa alimia 4 uliyotolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na  Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wanawake, vijana pamoja na walemavu. 

Wananchi wa Kata ya Maruvango  wamekuwa  na changamoto  mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana,kutopata mkopo  kutokanana  kukosa namba ya nida na vikundi vyao kuto kusajiliwa hivyo wameomba serikali iweze kuwasaidia  kutatua changamoto hizo,miongoni mwa wahitaji wa kupata mkopo Janeth urio kutoka kijiji cha mbasemi kata ya maruvango 

Huku Diwani wa Kata ya Maruvango  Majola Godson akamuomba  Mwenyekiti wa UWT kuzifanyia kazi changamoto za kata hiyo hususani   upatikanaji wa Huduma  bora katika Zahanati hiyo.
Share To:

Post A Comment: