Na,Jusline Marco;Arumeru

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Dkt.John Danielson Pallangyo amesema kuwa serikali inatambua mchango wa makanisa kwa jamii katika kuwajenga wananchi kiroho na kimaadili. 

Dkt.Pallangyo ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Spita wa bunge la Tanzania Mhe.Tulia Ackson katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la Waadventisa Usharika wa Usa river ambapo amesema kama Taifa litakuwa na watu walio na maadili ni rahisi kuwa na taifa lenye watu walio na tabia njema.

Ameongeza kuwa taasisi za dini zina mchango mkubwa katika kuisaidia serikali kutekeleza majukumu yake kwenye jamii,kama ujenzi wa shule,hospitali na miradi mingine mbalimbali ya kimaendeleo.

Aidha ametumia fursa hiyo kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea katikati ya jamii ikiwemo ulawiti na kesema kuwa serikali iko mstari wa mbele kupinga ndoa za jinsia moja ikiwa ni pamoja na kupinga ukatili wa kijinsia ili kuweka jamii katika maadili.

Kwa upande wake Askofu wa kanisa la Waadventista kutoka Jimbo la Kanda ya Bonde la Ufa  Dkt. David Mpwani amesema kuwa nyumba za ibada ni huduma za jamii kwa wananchi kwa kutoa maadili mema.

Harambee hiyo ya ujenzi wa kanisa hilo imetokana na jengo lililopo kutokidhi mahitaji ya ibada kutokana na wingi wa waumini.


Pichani wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Dkt.Danielson Palangyo,katikati ni Askofu wa kanisa la Waadventista kutoka Jimbo la Kanda ya Bonde la Ufa  Dkt. David Mpwani ,na wa mwisho ni Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Waadventista Usharika mdogo wa Usa river Reuben Steven Lomay, wakisikiliza ujumbe mbalimbali uliokuwa ukitolewa kwa njia ya uimbaji.
Askofu wa kanisa la Waadventista kutoka Jimbo la Kanda ya Bonde la Ufa  Dkt. David Mpwani akihubiri katika ibada ya harambee ya ujenzi wa kanisa la Waadventista (WASABATO) Usharika wa Usa river Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Dkt.Danielson Palangyo akiwapungia waumini wa kanisa la Waadventista katika ibada ya harambee ya ujenzi wa kanisa hilo, usharika wa usa river.
Share To:

JUSLINE

Post A Comment: