Na Mwandishi wetu. Mererani/ Simanjiro

Sakata la vurugu zilizoibuka ndani ya Mgodi wa Tanzanite wa kampuni ya Gem and Rock Venture unaomilikiwa mfanyabiashara maarufu, Joel Saitoti ,limechukua sura mpya mara baada ya meneja wa mgodi huo, kuibuka na kudai kuwa Mkaguzi wa baruti Ndg Ezekiel Issac aliwavamia wakiwa na watu zaidi ya 35 na kuwashambulia kwa kipigo na kisha kunyang'anya madini kinyume cha sheria.

Akitoa ufafanuzi wa sakata hilo,lililotokea machi 13 mwaka huu,meneja wa mgodi huo Martin Msigwa alidai kuwa siku ya tukio wakiwa wanaendelea na uzalishaji wa madini hayo ndipo walipo muona mkaguzi huyo wa baruti Ndg Ezekiel Issack akiwa ameambatana na wachimbaji wengine kutoka kitalu C waliwavamia na kuanza kuamuru wapewe madini hayo waliyokuwa wameyapata siku hiyo ambayo inakadiliwa kuwa na uzito wa zaidi kilo nne.

Alisema kabla ya Jopo hilo kufika, alikuja mkaguzi wa baruti, Ezekiel Isaac ambaye alifanikiwa kuvunja geti la Mtobozano akipitia mgodi wa Franone Mining na kuingia kitalu B inayomilikiwa na kampuni ya Gem and rock bila kufuata taratibu .

"Baada ya kufika walikuta shughuli za uzalishaji zikiendelea na kutaka wapatiwe madini wakilazimisha yapitie mgodi wa Kitalu C,lakini vijana wetu waligoma ku8achia madini hayo wakidai sio utaratibu wa kawaida kwakuwa mkaguzi wa baruti alikuwa mwenyewe alishirikiana na wafanyakazi wa Franone ,bila kuwepo askari polisi,jeshi la wananchi (JWTZ) na usalama wa taifa kama ilivyozoeleka"

Naye meneja msaidizi wa mgodi huo,Enock Nanyaro alidai kuwa kabla ya tukio hilo Machi 10 mwaka huu majira ya saa 10 jioni alipokea barua iliyotumwa kupitia mtandao wa WhatsApp kutoka kwa afisa mkaguzi wa baruti Ezekiel Isaac kwenda kwa meneja Nanyaro ikiitaka kampuni hiyo kusimamisha shughuli za uzalishaji katika Kitalu B ili kupisha uchunguzi baada ya kuwepo malalamiko ya kuwepo kwa hewa chafu inayotokana na mlipuko wa baruti kutoka kitalu B kwenda kitalu C kitu ambacho kinaweza kuhatarisha afya za wachimbaji wa kitalu C.


Nanyaro alisema kuwa uongozi wa mgodi huo uliamua kujibu barua hiyo kwa njia hiyo hiyo ya whatsApp wakimweleza Mkaguzi huyo kuwa umbali waliopo ni zaidi ya mita 580 kutoka mgodi wa Franone kwa hiyo sio kweli kwamba moshi wa baruti unawafikia.

"Tunashangaa kuona kampuni ya Franone wakilalamika kuhusu moshi wa baruti wakati wapo umbali mkubwa na sisi kama ni hivyo kwanini migodi mingine ya jirani kama mgodi wa Deo Minja ,Sunday na Papaking hawalalamiki"???

Naye Wilbart Mosses mfanyakazi wa mgodi huo wa Gem and Rock Ventures amesikitishwa kuona mkuu wa usalama Mererani (DCO) kutoa amri kwa askari aliokuwa ameongozana nao kuanza kuwashambulia kwa kipigo kikali na kupokonywa madini yetu ambayo ndio ujira wetu na kuondoka nayo.

Mosses alimwomba Rais Samia suluhu Hasan kuingilia kati sakata hilo ili kupata haki yao ya msingi kwani wamechoka kuonewa mara kwa mara pindi wanapoanza uzalishaji wa madini.

Kwa upande wake mmoja wa wachimbaji madini ya Tanzanite kutoka Mgodi wa kitalu B, Ndg Daniel Mollel anasema kwamba siku ya tukio yeye ndiyo alikuwa zamu katika kitengo cha uchukuaji madini kutoka machimboni kwenda duniani na kukabidhi kwa bosi wake kisha kukabidhi kwa serikali lqkini chq kushangaza aliishia kuambulia kipigo na kuokolewa na askari polisi.

"Nilivyotokea juu tu niliulizwa umebeba nini nikawaeleza nimebeba madini ambayo nampelekea fogo na afisa wa serikali ndipo nilipigwa kibao cha moto hadi nikaanguka chini na nilivyo nyanyuka tu nikapigwa kingine cha jichoni hadi sasa kama mnavyo ona jicho langu ndg wanahabari niliumizwa sana na ndipo nilipo nyang'anywa yale madini mkoni". Amesema Mollel.

"Baada ya kunyang'anywa yale madini ndipo kipigo kilikuja mfulululizo aliye ni okoa ni askari polisi baada kupiga kitako cha bunduki chini na kuwazua wale wengine waliyo kuwa wananipiga na kuwauliza kosa langu ni nini hadi napigwa kiukweli asingekuwepo askari polisi leo hii nisinge kuwepo maana nimepigwa mwili mzima hadi sehem zangu za sili haziko vizuri hadi sasa". aliongeza Mollel.

Share To:

Post A Comment: