Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Idara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara hiyo.


Sehemu ya watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara yao na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara hiyo. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara hiyo, Bi. Leila Mavika.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akipokea Mwongozo wa Mavazi kwa watumishi wa umma toka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili, Bi. Leila Mavika mara baada ya Naibu Waziri huyo kuhitimisha kikao kazi chake na watumishi wa Idara hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.


Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya Ukuzaji wa Maadili, Bw. Ally Ngowo akiwasilisha taarifa kwa Naibu waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete ya utekelezaji wa majukumu ya sehemu anayoisimamia (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Maadili kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI Mtumba jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.
Share To:

sayarinews.co.tz

Post A Comment: