Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Profesa Shadrack Mwakalila leo amekutana na kufanya Mazungumzo na Wahariri na Waandishi wa Habari kwa lengo la kuelezea baadhi ya Mafanikio ya Chuo katika kipindi cha Miaka Miwili ya Serikali ya Awamu Sita Madarakani.

Profesa Mwakalila ameeleza kuwa katika kampasi ya Kivukoni Chuo kimeboresha Miundombinu katika Mabweni ya Wanafunzi, Madarasa pamoja na ofisi za Wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kuweka umeme jua kwenye mabweni na kwenye barabara, kukarabati nyumba za Wafanyakazi na kanteeni na kuboresha mfumo wa majitaka.

Amesema Katika Kampasi ya Kivukoni kazi ya ujenzi wa maktaba kubwa yenye uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 2,500 pamoja na ukumbi wa mihadahara wenye uwezo wa watu 1000, ujenzi unaendelea vizuri upo asilimia 30. Fedha iliyotumika ni Bilioni 2.Katika Kampasi ya Karume, kazi ya ujenzi wa mabweni yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 1536 inaendelea. Fedha zilizotolewa na serikali ni Bilion 2.

Amesema Katika kampasi ya Pemba, kazi ya ujenzi wa madarasa na jengo la Utawala itaanza mwanzoni mwa Aprili 2023. Bilion 2.6 imetengwa kwa ajili ya ujenzi.Sera ya Uthibiti Ubora imehuishwa ili kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa ni bora na yenye viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa.

Chuo kimeendelea kutumia mtandao wa wireless (WIFI) na kuimarisha utumiaji wa mtandao kwa kuongeza kasi ya mtandao kutoka 36mbps hadi 236mbps.

Aidha, Zoezi la kuandaa mitaala mipya na kuhuisha mitaala ya zamani limekamilika ili kuwa na mitaala inayozingatia mahitaji halisi ya kitaifa na kimataifa. Katika maboresho hayo somo la uongozi, maadili, na uzalendo limeingizwa katika Mitaala yote ili kila mwanafunzi awe na ufahamu wa kutosha kuhusu uongozi, maadili, na uzalendo.

“Kumekuwa na ongezeko la idadi ya programu za mafunzo ambapo kwa sasa zimefikia Programu 32. Programu hizo ni kwa ngazi ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma), Shahada za Awali na Shahada za Umahiri. Udahili umeogezeka kutoka wanafunzi 11,413mwaka 2020/2021 hadi 14,457 mwaka 2022/2023.”Alisisitiza Profesa Mwakalila.

Amesema Chuo kimewezesha wahadhiri 56 kwenda kwenye mafunzo kwa ngazi mbalimbali za masomo ikiwemo Shahada ya Uzamivu, Shahada ya Umahili, Shahada ya Awali na Stashahada na Chuo kimefanya mafunzo kupitia semina ya mbinu za ufundishaji kwa wahadhiri wote wa Kampasi zote, Pia Chuo kimeongeza idadi ya walimu/wahadhiri wenye shahada ya uzamivu (PhD) kutoka wahadhiri 37 kwa mwaka 2020 hadi wahadhiri 46 mwaka 2023.

Profesa amesma Idadi ya watumishi imeongezeka baada ya kupata kibali cha ajira za wahadhiri 86 na kufanya jumla ya watumishi wa kudumu kuwa 305. 

Aidha, Chuo kimekuwa na bunifu zaidi ya bunifu 22 na zimeshindanishwa kwenye maonesho mbalimbali ambapo kati ya bunifu hizo bunifu moja ilishika nafasi ya pili kitaifa katika mashindando ya maonesho ya Kitaifa ya Sayansi Tekinolojia na Ubunifu (MAKISATU) na Nyingine ilishika nafasi ya nne kitaifa.

 

Imetolewa na;

KITENGO CHA HABARI NA MAHUSIANO

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

17.03.2023

Share To:

Post A Comment: