Rose Kagoro meneja ushawishi kutoka Railway Children Africa akizungumza katika mafunzo ya namna Bora ya kupunguza athari kwa watoto wanaoishi kwenye makao ya watoto.
Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto,mameneja wa vituo vya kulelea watoto na maafisa ustawi wa jamii Mkoa wa Iringa na Njombe katika picha ya pamoja kwenye mafunzo ya kuwakinga watoto na athari zinazotokea katika vituo vya kulelea watoto.

Na Fredy Mgunda, Iringa.


WASIMAMIZI,Mameneja wa vituo vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi Mkoa wa Iringa na njombe wamepewa mafunzo ya  namna bora ya kupunguza athari kwa watoto wanaoishi kwenye makao ya watoto (Vituoni) ikiwa ni pamoja na athari za kukosa malzi kutoka katika familia  

Akizungumza katika mafunzo hayo Hannes Sandahl amesema kuwa baadhi ya watoto wanaoishi katika vituo vya watoto  wamekuwa hawapati malezi ya kitanzania yenye kumuandaa mtoto kuishi maisha yaliyopo kwenye jamii hali inayopelekea mtoto kukosa upendo pamoja na kupata changamoto ya kisaikolojia na kujiona tofauti .

Kwa upande wake Subilaga Mwaigwisya afisa ustawi wa jamii mkoa wa Njombe amesema kuwa changamoto ya wazazi kuacha jukumu la malezi kwa jamii linasababisha mmomonyoko wa maadili huku akiwashauri walezi wa vituo vya kulelea watoto kuwarudisha nyumbani watoto ambao kesi zao zimeamriwa kisheria ili kumrudisha mtoto katika malezi ya familia

Subilaga alisema kuwa katika mkoa wa njombe walibaini vituo vya kulea watoto wamkuwa wakipokea watoto bila kufanya mawasiliano na afisa ustawi hali inayopelekea kutotambua watoto wametoka katika familia ipi na namna gani anawea rudishwa nyumbani huku asilimia 75 ikionekana watoto walio na mzazi mmoja

“Watoto hawa wengi wao wanakuwa na mzazi mmoja kama asilimia 75 a watoto waliopo katika makao wanamzazi mmoja kama ni baba au mama na chnagamoto ni kwamba mamneja wa vituo wanapokea watoto bila kuwasiliana na ustawi ndo maana tunapata changamoto jinsi ya kuwarudisha katika familia zao “

Oggu Nanyaro ni katibu wa mafunzo kutoka Small Things Tanzania alisema kuwa wamekuwa wakihakikisha mtoto anapata malezi kutoka kwa wazazi huku akisema makao ya watoto yamefanyika kama mbadala wa kwanza hali ambayo inepelekea ukatili kwa watoto kisaikolojia .

“ Tumekuwa tukiboresha mifumo ya watoto kwanza kuhakikisha mtoto anapata malezi bora na kukua ndani ya familia pia tunazuia watoto kwenda katika makao ya watoto tunatakiwa tutatue changamoto zilizotokea ili mtoto huyu arudi ndani ya familia aishi katika malezi ya familia changamoto kubwa makao ya watoto yamefanyika kama mbadala wa kwanza pia tulibaini uwepo wa wawahudumu wasio na sifa ili hali inatakiwa kwenye vituo kama ikiwezekana wawepo wahudumu waliosomea mambo ya afisa ustawi “

Naye Rose Kagoro  meneja ushawishi kutoka Railway Children Africa alisema kuwa mchakato wa mashauri ya kesi za watoto ufanyike kwa wakati pamoja na kupata maelezo kutoka pande mbili kwani kuna watoto ambao wamekuwa wakitoa taarifa zisizo za kweli ili watoke ndani ya familia

“ Tulienda masokoni kutoa elimu ili jamii isimamie suala la malezi vizuri ingekuwa vyema mchakato wa mashauri ya serikali yafuatwe , tathmini ifaqnyike ili kujua watoto hawa wanahitaji nini pia lazima upate taarifa kutoka pande zote mbili kwa sababu kuna watoto wamekuwa wakidanganya lakini tunashukuru vyombo vya habari pamoja na changamoto zake vimekuwa vikitusaidia kupata ndugu wa watoto ambao hawafahamu kwao “ alisema Rose

Brown Emmanuel Mratibu wa Uchumi Miradi na Maendeleo kutoka kanisa la KKKT  alisema kuwa serikali imetazamia mikoa miwili ambayo ni mkoa wa Iringa na njombe huku kwa kanisa la KKKT ni dayosisi nne dayosisi ya kusini ,dayosisi ya kusini kati dayosisi ya kusini magharibi .

Mafunzo hayo yamewakutanisha  mameneja ,wamiliki wa vituo na maafisa ustawi ili kupunguza makali kwenye malezi  ya mtoto hasa kwenye vituo vya kulelea watoto na kupitia miongozo ya serikali iliyotolewa

MWISHO .


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: