Na Denis Chambi, Tanga.
 
Halmshauri ya jiji la Tanga  imetenga eneo lenye ukubwa  hekari  mia mbili kwaajili ya kilimo ambalo wanatarajia kuligawa kwa vijana wapatao 200 ili waweze kujishughulisha na Kilimo kwa lengo la kuwasaidia  kujikwamua kiuchumi.

Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dkt. Sipora Liana amesema kuwa eneo hilo ambalo lipo Mleni kata ya Mabokweni bado ni pori wanatarajia kulisafisha kwa kushirikiana na shirika la Botner Foundation tayari kwa ajili ya kuligawa kwa vijana hao.

Alisema kutokana na jiograhia ya Tanga aridhi yake ambayo inastawi mazao mbalimbali itasaidia sana kuufungua mkoa huo kupitia sekta ya kilimo  hii ikienda kuakisi kwa vitendo kauli mbiu ya sasa inayosema  'Tanga lango kuu la uchumi Afrika Mashariki'.

"Tumeweza kupate eneo la hekari mia mbili  tutalisafisha tukishirikiana na  shirika la Botner foundation  tuweze kuwagawia vijana zaidi ya mia nane waweze kulima,  tunajua sisi Tanga tuko kwenye lango la uchumi wa Afrika Mashariki tukipanda  mazao yeyote yale ni rahisi sana kusafirishwa,   mheshimiwa Rais katuboreshea bandari yetu  ya Tanga ambayo itakuwa ni rahisi sasa  kupeleka mazao yetu visiwa vya Comoro,  Pemba au Unguja mazao yeyote tunajua watu wa maeneo haya wanakuja kuchukua mboga mboga hapa Tanga" alisema Dkt Liana.

Alisema katika kuimarisha zaidi sekta ya kilimo katika eneo hilo halmashauri hiyo imejipanga kuweka miundo mbinu ya umwagiliaji hatua ambayo itawasaidia  vijana hao  kwa asilimia kubwa na hivyo kuweza kuchangia pato la Taifa na kujipatia kipato.

"Sisi jiji la Tanga tumedharia katika hilo eneo la hekari mia mbili tutaweka  miundombinu kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji kwahiyo vijana wetu watagaiwa na tunaamini kwamba    wimbi la vijana ambao hawana watapata  shughuli za kufanya,  tunaamini mpaka ikifika 2025 tutakuwa sehemu nzuri" aliongeza.
Aidha alimpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo halmashauri hiyo ilipokea shilingi Million 540 kwaajili ya ujenzi wa soko jipya la wamachinga katika Soko la Mlango wa Chuma  ambalo bado ujenzi wake unaendelea hadi sasa.

" Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  mwishoni mwa mwaka jana 2022 alileta fedha Million 540 kwaajili ya kujenga soko jipya la wamachinga  lile soko tunaendelea nalo pale na tumefika hatua nzuri sasa hivi sisi Halmashauri tumeongeza mapato ya ndani  shilingi 360 ili kuweza kuendeleza pale ambapo soko limeishia kwa sababu soko lenyewe ni kubwa na wamachinga waliopo ni wengi" aliongeza Dkt. Liana.

Sambamba na hayo halmashauri ya jiji la Tanga ilipokea kiasi cha shilingi 470 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata ya   Magaoni   wakimshukuru na kumpongeza  Rais  Samia Suluhu Hassan  kwa hatua  hiyo ikiwa ni miaka miwili imetimia katika awamu ya sita  ya utawala wake.

"Lakini pia Mheshimiwa Rais ameleta Million 470 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya Magaoni ile shule ina kila kitu  imejengwa maabara maktaba  na miundombinu mingine lakini ameleta pia milion 450 kwaajili ya ukarabati wa shule ya sekondari ya Usagara  na Million 500 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Tongoni" aliongeza.

Dkt Liana aliongeza kuwa  wamekuwa wakitekeleza kwa vitendo agizo la serikali katika usimamizi wa ukusanyaji mapato  ya ndani ambapo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 jiji la Tanga lilivuka lengo kwa kuweza  kukusanya  Billion 17  ambapo lengo walilopangiwa  lilikuwa ni Billion 15 na mwaka huu wakipangiwa kukusanya Billion 18 mpaka December 2022 wakiwa  tayari wamefikia asilimia 50.


Share To:

Post A Comment: