Na Denis Chambi,  Tanga.
Milango
 ya kibiashara  na kiuchumi hapa nchini kupitia bandari ya Tanga inazidi
 kufunguka hii ni mara baada ya Meli  yenye ukubwa wa mita 189.9 kutia 
nanga hivi karibuni  ikitokea Marekani katika bandari ya Portlex  ikiwa 
imebeba shehena ya  malighafi aina ya Petcoc  tani 51  kwaajili ya 
viwanda vya Sayona na  Neelkanth vilivyopo jijini Tanga.
Kufwatia
 maboresho yaliyofanywa na serikali yaliyoghalimu Jumla ya shilingi 
bilioni 429.1 zilizotumika katika mradi wa maboresho  ya gati mbili 
zenye urefu wa mita 450 na kuongeza kina cha bahari    kwa lengo la 
kuiwezesha bandari hiyo kuhudumia meli kubwa ambazo awali hazikuweza 
kushusha mizigo moja kwa moja bandarini hapo kutokana na kina kidogo.
Maboresho
 hayo yaliyofanyika ambayo ni gati mbili zenye urefu wa mita 450 
zilizojengwa miaka ya 1914 na 1958  pamoja na kuongeza  kina cha bahari 
kutoka mita 13 hadi13 ambazo sasa zinawezesha meli kubwa mbili na 
kuhudumiwa kwa wakati mmoja.
Akizungumza
 mara baada ya kuipokea Meli hiyo mkuu wa kitengo cha masoko katika 
bandari ya Tanga Rose Tandiko amesema kuwa   Meli hiyo ya MV Motsovo  ya
 mizigo ni kubwa zaidi ya zile ambazo zilishawahi kupokelewa bandarini 
hapo na bado wanaendelea kupokea nyingine akitumia nafasi hiyo 
kuwakaribisha wadau na wafanyabiashara wa ndani na nje ya Tanzania 
kuendelea kuitumia bandari hiyo
"Leo
 tumepokea meli kubwa kuwahi kuhudumiwa katika bandari yetu ya Tanga  
ambayo imekuja kutokea nchini Marekeani ikiwa na mzigo wa Petcoc tani 
elfu 51 kwaajili ya viwanda vya Neelkanth na Sayona limited,  huu n 
mwanzo tu wa huduma zilizotukuka katika bandari ya Tanga bado 
tutaendelea kuhudumia meli nyingine mbili kubwa gatini kwa wakati mmmoja
 kama matakwa ya ujenzi wa gati letu"
"Tuwahamasishe 
 wadau wa bandari ya Tanga,  wadau wa bandari  zote hapa nchini na 
kweingineko kwamba endeleeni kutumia bandari yetu  bandari ya Tanga kwa 
sasa tunaweza kusema imenoga huduma zimetukuka na utendeaji kazi ni 
mzuri hivyo tunawakaribisha sana kutumia bandari yetu ya Tanga" alisema 
Tandiko.
Meli hiyo 
iliyopokelewa bandarini  Tanga  march 18 ilitokea katika bandari ya 
Portlex nchini malekani february 3, 2023 kwaajili ya kuleta shehena hiyo
 ya Petcoc  inatoyumika kwenye viwanda vya Sayona na Neelkanth kama 
chanzo cha moto wa viwandani
Meneja
 usafirishaji  kutoka kampuni ya Seif Issa MR & SONS ambao ni 
miongoni mwa wadau wa bandari ya Tanga  ameipongeza  serikali kwa 
uwekezaji mkubwa uliofanyika katika kuboresha na kuweka mazingira kwa 
rafiki kwa  wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo wa kutoka nje na 
ndani ya nchi ambapo itawasaidia kwa kiasi kikubwa  tofauti na hapo 
awali.
"Tunataraji 
utendaji kazi mzuri kwa sababu kila idara imejipanga kuanzia wafanya 
kazi na vitendea kazi kwahiyo tunategea tufanye kazi kwa siku ambazo 
tumepangiwa , wafanyabiashara wasihofie wala kuogopa  tunaamini bandari 
iko salama kabisa kila kitu wamekiweka katika mpangilio mzuri kwahiyo 
wadau wengine  tunaomba waitumie bandari ya Tanga" alisema Issa.
Tangu
 kufanyika kwa maboresho ya ukarabati wa gati mbili na upanuaji wa kina 
cha bahari bandari hiyo imeendelea kuvunja rekodi za kupokea meli kubwa 
za mizigo kutoka nje ya nchi  ambapo kabla ya Mv Metsovo zilitia nanga 
meli zenye urefu Mita 150,  na 179  kwa nyakati tofauti tofauti hii 
ikiendana na kauli ya Tanga lango kuu la uchumi Afrika mashariki.

Post A Comment: