Na Denis Chambi, Tanga.
 
MWENYEKITI  wa Chama cha Demokrasia  na Maendeleo CHADEMA kanda ya Kaskazini Godbless Lema ameendelea kusimamia kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kuwa shughuli ya madereva waendesha pikipiki maarufu kama Boda boda sio kazi badala yake inauwa nguvu kazi ya Taifa la kesho akisistiza kuwa bado kundi hilo ni janga lililopo hapa nchini wengi wakishindwa kuyamudu maisha wanayoishi na familiya zao. 

Lema ameendelea kusisitiza kauli hiyo akiwa mkoani Tanga march 20 , 2023 katika mkutano wa hadhara ikikumbukwa kuwa mara tu alipowasili hapa nchini  january 2023 akitokea  Canada alikokuwa tangu mwaka 2020,  ambapo mara baada ya kukutana na mamia ya wafuasi wa chama hicho mkoani Arusha aliizungumza na hatimaye kuibua baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa pamoja na uongozi wa Bodaboda wakimtaka akanushe kauli yake na kutokuibize  kazi hiyo lakini bado ameonyesha  msimamo wake.

"Nasema sifuti kauli na leo tena  napigilia  msumari kuwa udereva boda boda sio kazi  ya maana na watu wanazidi kuwa masikini na hii inajenga ufukara, bodaboda zimeongeza vilema  na wajane  leo hii kuna watu wanapoteza ndugu zao na maisha kwa sababu ya ajali za boda boda ,  " alisema Lema

Aidha Lema ameeleza kuwa kuna athari ambazo zinaweza kujitokeza hapo baadaye kutokana na wazazi walezi na jamii kwa ujumla kushindwa kuwalea watoto katika maadili mema jambo ambalo linaweza kuchoche kushamiri kwa vitendo vya ukatili sambamba na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.

" Watoto wengi wanaozaliwa sasa hivi hawalelewi na wazazi wao ipasavyo kama nyakati za wazee wetu  je! Hivi meangalia taifa hili baada ya miaka 30 nchi itakuwaje nyie? ndio maana sasa hivi tunashangaa kuna tabia zinazuka umasikini umekuwa mkali kuwanyima  nafasi kwa wazazi kuwaangalia watoto" aliongeza Lema.

Awali akizungumza mjumbe wa halmashauri kuu ya CHADEMA Taifa Grace Kiwelu  alimpongeza  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa hatua aliyochukuwa ya kufungua  milango na kuridhia mashirikiano baina ya vyama vyote vya siasa pamoja na kuruhusu mikutano ya kisiasa  akisema kuwa licha ya hayo yote bado CHADEMA itaendelea kusimamia msimamo wake kuhubiri umuhimu wa kupatikana kwa katiba mpya.

"Niwashukuru sana viongozi wetu wa vyama viwili wa Kitaifa wa Chama Cha Mapinduzi 'CCM'  na  Chama cha Demokrasia na Maendeleo 'CHADEMA' kwa kuleta maridhiano leo watanzania tunazungumza ,  tumekuwa kwenye lifungo cha miaka saba bila watanzania kuzungumza"

Mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya  kata ya Msambweni ulihudhuriwa pia na aliyewahi kuwa Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi 'MNEC'.

Pamoja na hayo chama hicho kimtembulisha uongozi mpya wa CHADEMA ngazi ya wilaya ukiongozwa na Rashid Jumbe ikikumbukwa kuwa katika ziara ya mwenyekiti taifa  Freeman Mbowe aliyoifanya hivi karibuni mkoani Tanga aliuvua madaraka uongozi uliopo na kuwachagua wengine hii ikilenga hasa kuzidi kukiimarisha chama hicho kuanzia ngazi za chini.

Uongozi huo mpya unaoongozwa na aliyekuwa mwanachama wa ACT Wazalendo na ambaye baadaye kuhamia CHADEMA kwa sasa akikaimu nafasi ya mwenyekiti  , Khalid Hamza kaimu katibu,  Shaban Ngozi aliyeteuliwa kuwa  katibu mwenezi wa chama hicho, Zima Mohammed akikaimu nafaai ya baraza la wazee,   Zena Khamis kaimu mwenyekiti Bawacha,  Amos Chiluda Mwenyekiti wa wazee Selestin Kiria mweka hazina wa jimbo na wengine wengi waluokaimu nafasi zilizoachwa wazi mara baada ya mabadiliko kitoka uongozi uliopita.
 

Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Grace Kiwelu akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa CHADEMA (kushoto) mkoa wa Tanga akisalimiana na aliyewahi kuwa MNECwa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Tanga ambaye walimualika katika mkutano huo.
Uongozi mpya wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilaya ya Tanga uliotambulishwa rasmi katika mkutano wa hadhara wa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini Godbless Lema uliofanyika mkoani Tanga March 20,2023.
 


Share To:

Post A Comment: