Na; Elizabeth Paulo, Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule amepongeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA kwa ubunifu mkubwa wa madaraja ya mawe ambayo yatasaidia kupunguza bajeti kwa asilimia 50%.


Senyamule ametoa pongezi hizo leo Machi 16 Jijini Dodoma wakati alipokua Mwenyekiti katika Kikao cha Bodi ya Barabara huku akisema ubunifu huo ni mzuri kwani badala ya kujengwa Daraja moja yatajengwa madaraja mawili.


Sasa huko ndio twende hatuna sababu maeneo ambapo yanafaa Madaraja ya mawe tukajenga yale mengine hasa ukizingatia uimara na ubora ni uleule, Kwahiyo tuone matumizi ya hayo madaraja ya mawe unaendelea kuimarishwa. Alisema Senyamule




Aidha Senyamule ameitaka bodi ya Barabara ya mkoa kuendelea kusimamia Barabara zinazojengwa na ambazo zimejengwa ili ziendelee kudumu na bodi ihakikishe inawafikia Wananchi kwa huduma za Barabara


Kadhalika Senyamule ameitaka bodi hiyo ya Barabara mkoa kutoa elimu kwa madereva wa magari makubwa (Malori) kuacha kupaki magari pembeni mwa Barabara na kupeleka Barabara hizo kukatika badala yake kupaki sehemu ambapo ni rasmi.


Awali akiwasilisha taarifa ya Wakala Wa Barabara za Vijijini na Mijini Meneja wa TARURA mkoa wa Dodoma Eng. Lusako Kileme amesema kupitia wadau mbalimbali, TARURA ina mpango wa kutekeleza miradi mbalimbali kwa kutumia teknologia mbadala ili kupunguza garama za utekelezaji wa miradi zinazodumu kwa muda mrefu.



Teknologia hizi ni ECOROADS, POLYMER, na Matumizi ya mawe katika ujenzi wa Madaraja.Alifafanua Eng.Kileme


TARURA upande wa Dodoma tumeanza kutekeleza ujenzi wa madaraja ya mawe na kuna baadhi ya mafundi wameshaenda Kigoma kupata Mafunzo na Dodoma tuliteua na wameenda mafundi saba (7) na wameanza wiki hii watakaporudi watafundusha wenzao lakini tutawapatia hizi kazi za kujenga madaraja ya mawe. Alielezea Eng. Kileme


Eng.Kileme amesema Kwenye bajeti ya mwaka huu kuna baadhi ya maeneo yametengwa kwaajili ya kuanza ujenzi wa madaraja hayo ya Mawe.


Pale tunapoona sehemu ambayo malighafi ya mawe yanapatikana na kwa urahisi tutatumia na tutajenga madaraja ya mawe. Alisema Eng. Kileme


Aliongeza Tutaendelea kuwapa Mafunzo mafundi na wahandisi waliopo kwaajili ya kufanya usanifu lakini pia kwenye usimamizi wa ujenzi wa madaraja hayo. Aliongezea


Katika hatua nyingine Eng. Kileme amesema TARURA mkoa wa Dodoma wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi hivyo kuwatumia wahandisi wa vyuoni wanaofanya mafunzo maalumu na kusaidia kupunguza changamoto hiyo.


Aidha Bajeti imeendelea kupanda ndani ya miaka miwili tifauti na miaka mitano iliyopita ambapo mpaka sasa takribani asilimia zaidi ya Mia tatu (300) kwa mkoa Kutoka bajeti ya wastani wa Bilioni ishirini (20) Kwenda Bilioni hamsini na tano (55) Kwa upande wa TANROAD na TARURA.




Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: