Na Denis Chambi,  Tanga.

Matokeo chanya ya maboresho yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan  katika bandari ya Tanga yanaendelea kuonekana kufwatia meli kubwa za mizigo kutoka nje ya nchi  zikiendelea kutia nanga wafanyabiashara wakizidi kuitumia hatua ambayo inakwenda kuongeza biashara shindani katika ukanda wa Afrika mashariki.

Ukiachana na meli kubwa iliyopokelewa hivi karibuni imeendelea kuwa mwendelezo ambapo bandari hiyo imepokea nyingine yenye urefu wa mita 150 kutoka china iliyobeba Clinka ya kiwanda cha Lime stone kilichopo mkoani hapa huku wakitarajia kupokea meli nyingine yenye urefu wa mita 189.9 hii ikionyesha mapinduzi ya kibiashara ambayo yatazidi kuifungua Tanga.

Bandari ya Tanga imeanza kuhudumia meli kubwa ya mizigo yenye urefu wa mita 179 meli ambayo imekuja na magari ikiwa ni mara ya kwanza kushushwa magari bandarini hapo baada ya maboresho ya ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 450.

Meli hiyo iliyotokea Nchini China ni meli ya kwanza kuja na magari katika bandari ya Tanga tofauti na meli nyingine ambazo zilishakwisha kutia nanga bandarini hapo mara baada ya kukamilika kwa maboresho hayo. 

Ukiachana na meli kubwa yenye urefu wa mita 150 iliyopokelewa hivi karibuni katika bandari ya Tanga imeendelea kuwa mwendelezo ambapo bandari hiyo kwa mara nyingine imepokea meli yenye urefu wa mita 179 kutoka Nchini China iliyobeba magari na vifaa vya kiwanda cha Maweni Lime stone kilichopo Mkoani hapa huku wakitarajia kupokea meli nyingine yenye urefu wa mita 189.9 hii ikionyesha mapinduzi ya kibiashara ambayo yatazidi kuifungua Tanga'.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea na kujionea utendaji kazi wa bandari hiyo mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba  aliyekuja na kauli mbiu ya 'Tanga lango kuu la Afrika Mashariki amesema kuwa wanaitazama bandari ya Tanga kimkakati zaidi na kuwaasa wafanyabiashara mbalimbali  wa kutoka ndani ya Tanzania  na  nchi za Afrika Mashariki kuitumia bandari ya Tanga ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwao katika kusafirisha mizigo yao kwa haraka zaidi.

 "Niwaombe wafanyabiashara wote wa ndani na nje ya Tanga kutumia bandari yetu ya Tanga lakini pia niwasisitize majirani zetu wa Rwanda,  Burundi,  Congo,  Kenya na kwingineko waangalie bandari ya Tanga  kama changuo lao namba moja, "alibainisha Kindamba. 

"Bandari hii ndio moyo wa uchumi wa Mkoa wa Tanga sisi kama wasimamizi wa serikali tunakwenda kuisimamia bandari hii kwa ukaribu zaidi tunataka Dunia ijue kwamba ipo bandari inayoitwa bandari ya Tanga tena ikiwa na usalama mkubwa kabisa, "alisisitiza Kindamba.

Aidha amewaomba wafanyabiashara mbalkmbali  wa kutoka ndani ya Tanzania  na  nchi za Afrika Mashariki kuzidi kuitumia bandari hiyo ambayo itakuwa na manufaa kwao huku akiwataka wa wafanyakazi wa bandari hiyo kuendelea kudumisha mahusiano baina yao.

"Kuwaomba wafanyabiashara wote wa ndani na nje ya Tanga kutumia bandari ya Tanga , kuwaomba majirani zetu Rwanda , Burundi Congo Kenya na kwingineko waangalie bandari ya Tanga  kama changuo lao namba moja na sisi tunakwenda kuisimamia bandari hii kwa ukaribu zaidi na ndani ya kupindi kifupi watu watakaa na kuizungumzia bandari ya Tanga ambayo haijawahi kuzungumzwa tena tutakuwa tunavunja rekodi zetu sisi wenyewe  kwa wenyewe,  tunataka dunia ijue kwamba ipo bandari inaitwa Tanga" alisema Kindamba.

Meneja wa bandari ya Tanga Masoud Mrisha pamoja na maboresho hayo yaliyofanyika ameiomba serikali kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA na TANROADS kutengenezwa kwa miundombinu ya barabara ya kilomita 7 inayokwwnda Mwambani kwenye bandari ndogo ambako wanatarajia kujenga

"Wote tunafahamu kwamba  bandari   ndio moyo  wa biashara kwa mkoa wa Tanga mkuuwa mkoa tulimwomba atusaidie ndungu zetu wa Tanroads na TARURA  kututebgenezea ile barabara kutoka hapa mpaka mwambani kilomita 7 kule tunatarajia kujenga sehemu ya kuhifadhia mizigo yetu  sote tunafahamu bandari yetu ya Tanva ina ukubwa wa hekta 17 eneo hili sio kubwa sana tumemwomba mkuu wa mkoa atusaidie kututilia nguvu kwenye hizo taasisi" alisema Mrisha.

"Niiombe Serikali kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarura na Tanroads kutengenezwa kwa miundombinu ya barabara ya kilomita 7 inayokwenda Mwambani kwenye bandari ndogo kule tunatarajia kujenga sehemu ya kuhifadhia mizigo yetu  sote tunafahamu bandari yetu ya Tanga ina ukubwa wa hekta 17 eneo hili sio kubwa sana tumemwomba mkuu wa mkoa atusaidie kututilia nguvu kwenye hizo taasisi" alisema Mrisha

Serikali imewekeza kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 429 kwenye bandari ya Tanga kwajili ya ujenzi wa gati,  kuongeza kina cha maji na ununuzi wa mitambo kwajili ya kuwezesha bandari hiyo kuhudumia meli kubwa ambazo zilikuwa zinashindwa kutia nanga bandarini hapo. 

Hata hivyo serikali inatarajia kufanya uzinduzi rasmi wa mradi wa gati katika bandaro hiyo ifikapo mwezi April mwaka huu. 
 
 
Meli yenye ukubwa wa urefu wa mita 179 ambayo imekuja na mzigo  magari na Clinca kutoka China ikiwa ni mara ya kwanza kutia nanga  bandarini hapo baada ya maboresho ya ujenzi wa gati mbili  zenye urefu wa mita 450.
 

Meneja wa bandari ya Tanga Masoud Mrisha akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba March 15 wakati alipotembelea kujonea utendaji kazi.
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza mara baada ya ziara yake ya kutembelea bandari ya Tanga na kuzungumza na wafanyakazi march 15, 2023. kushoto kwake ni meneja wa bandari hiyo Masoud Mrisha.

.


Share To:

Post A Comment: