Na Angela Msimbira OR- TAMISEMI


Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (iCHF) Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Silvery Maganza amesema  kati ya  shilingi bilioni 30.167 zilizokusanywa kupitia mfuko huo shilingi  bilioni 22.2  zimelipwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya

Akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa kwa kipindi cha mwaka 2018 hadi desemba, 2022 Maganza amesema kuwa mfuko umelipa asilimia 75 ya makusanyo yake katika vituo vilivyotibu wanachama.

Maganza amesema malipo hayo hufanyika kulingana ongezeko la wanachama ambapo mfuko ukiwa na wanachama wengi thamani ya dai linaongezeka.

Akitolea mfano wa Mkoa wa Dar-es-salaam amesema  dai limepanda kutoka Tsh 13,992 mwaka 2019 hadi Tsh 103,255 mwaka 2022 ambapo mpaka sasa jumla ya vituo  binafsi 15 vimeingia makubaliano ya huduma. 

Ameendelea kusema kuwa CHF iliyoboreshwa imeweza kubeba kaya za wasio na uwezo na kuchangia katika kupunguza mzigo wa misamaha ya matibabu na kuwezesha  makundi yote ya kijamii kuzifikia huduma za ma tibabu kwa usawa (equitable access) bila changamoto ya kifedha.

Naye, Mratibu wa CHF iliyoboreshwa  Francis Lutalala amesema  jumla ya wanachama  403,656 wamesajiliwa  kwenye mfumo wa CHF iliyoboreshwa kwa kipindi cha Julai 2018 hadi Desemba, 2022.

Aidha,amesema katika Kipindi cha Julai hadi Novemba 2022 Kituo cha Afya Makole kimelipwa shilingi 95,310.14 ambapo fedha hizi zimetoka Mikoa ya Dar es Salaam,Tabora, Ruvuma, Singida, Njombe, Mwanza na Pwani.

Share To:

Post A Comment: