Na John Walter-Babati

Serikali imeagiza kufanyika uchunguzi wa mfumo wa uagizaji, Utunzaji na Utoaji wa dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara baada ya kubaini mianya ya upotevu wa dawa kwenye hospitali hiyo.

Hayo yamesemwa  na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk Festo Dugange wakati akiwa ziara ya kikazi mkoani hapa ambapo aliitembelea hospitali hiyo iliyopo kata ya Mwada.

Amesema Serikali imeweka utaratibu wa kuagiza dawa, kupokea, kutunza na kutoa dawa kwa wagonjwa lakini taratibu hizo hazifuatwi jambo ambalo linatoa mianya ya wizi katika hospitali hiyo.

Dk Dugange amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa Manyara ndani ya siku saba kuhakikisha anapeleka timu maalumu ya kufanya uchunguzi wa uagizaji, utunzaji na utoaji wa dawa ili hatua stahiki zichukuliwe iwapo itajiridhisha upotevu wa dawa.

Aidha alikagua barabara ya lami Ngarenaro Magugu ambayo ameridhika nayo, sule ya Sekondari Sarame pamoja na Zhanati ya Galapo.
Share To:

Post A Comment: