Diwani wa Kata ya Boma Julius  Kisoma akizungumza na waandishi wa habari eneo ambalo mkandarasi anasumba kukamilisha ujenzi.
Baadhi ya wananchi wa wanaopita barabara hiyo wakiwa wanakumbana na adha ya usafi wa kupita katika barabara hiyo.
Hii ndio barabara ambayo imekuwa ikileta madhara kwa wananchi wa kata ya Boma.


Na Fredy Mgunda, Iringa.

WANANCHI wa mtaa wa balali kata ya Boma Halmashauri ya Mji Mafinga wamelakamikia Mkandarasi wa kampuni ya Rahda Investment kushindwa kukamilisha mradi wa Ujenzi wa kipande cha barabara ya balali kwa wakati hali ambayo imepelekea kuleta adha kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.

Barabara hiyo inatokea sokoni kwenda kituo cha Afya ihongole kupitia mtaa wa balali ambapo  imekuwa kero kubwa kwao wananchi wa maeneo hayo hali ambayo iliwalazimu kupaza sauti zao ili waweze kusaidiwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi,Mkazi wa Ihongole na dereva Bajaji Patrick chang'aa amesema kuwa barabara hiyo imekuwa kero kubwa kwao kutokana na  Mkandarasi kushindwa kukamilisha kwa wakati hali ambayo inasababisha msongamano mkubwa kwenye barabara hiyo 


" Hii barabara imekuwa kero kwetu hasa kipande hiki cha balali kutoka sokoni kwenda kituo cha afya ihongole  sisi madereva ambao tunatoa huduma ya usafiri  Bajaji zetu zinaharika kwa sababu ya ubovu wa barabara hivyo tunaomba Serikali iingilie Kati kuhusu suala hili." Amesema Chang'a

amesema kuwa barabara hiyo inaumuhimu mkubwa kutokana wanasafirisha  watu mbalimbali na wagonjwa pamoja na  akina mama wajawazito kwa ajili ya  kuwapeleka kituo cha afya ihongole kupata matibabu.

" Huyu Mkandarasi ambaye amepewa hii barabara ametukosea sana kwa sababu akina mama wajawazito wanateseka  hata ukiendasha taratibu kwa namna barabara ilivyo hawezekani." Amesema Kinyanga

Naye Mmoja wa wakazi wa Ihongole Aloni Kinyaga amesema kuwa wanashindwa kupita vizuri kwa sababu Mkandarasi amepanga nawe kwenye barabara hiyo kea muda mrefu kwa kipindi cha miezi minne hadi sasa.

" Hii barabara mvua inaponuesha kupata adha kubwa ya kubadirisha vikombe kuharibika kwenye Bajaji zetu hii ni changamoto hata mzungo wa biashara umedorora kwa sababu ya abiria hawezi kupanda wakati anaona anateseka hivyo wanaona ni bora watembee kwa miguu kutokana na adha ambayo wanaipata kwenye barabara hiyo.." Amesema Kinyaga


Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Boma Julius  Kisoma amesema kuwa barabara hiyo ilitakiwa kakamilika januari 15 mwaka huu lakini hadi sasa bado haijakamilika.

Diwani hiyo amesema mikataba ya ujenzi wa barabara hiyo ulisainiwa na Wakala wa barabara za mijini na vijiji (TARURA) Mkoa wa Iringa  hivyo inakuwa vigumu kuwachukulia hatua.

" Hii ni changamoto kubwa kwetu kwa sababu hata tukienda kwa Meneja wa Tarura Wilaya anakuwa hana majibu  hivyo tunaomba Serikali iturudishie Mamlaka hizi ziwe chini yetu ili kupunguza malalamiko hayo na itaturahisishia jinsi ya kuzifuatilia tofauti  ilivyo sasa." Amesema Kisoma

Amesema baada ya wananchi kuona ujenzi huo umechelewa kukamilika walilazimika kuondoa mawe ambayo yalipangwa kwa ajili ya Ujenzi huo kuyaondoa ili waweze kupita kwa urahisi.

" Wananchi waliondoa mawe kwenye barabara hapa gharama zinaanza upya kwa sababu mawe walikuwa wameyapanga na ilibaki kazi ya kuweka kifusi tu ili wananchi waanze kupita kuendelea kufanya shughuli zao." Amesema kisoma

Akijibu kero hiyo Msimamizi wa barabara hiyo Mhandisi wa kampuni ya Rahda Investment Francis Mnyambogwe amesema sababu ya kuchelewa kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo ni kutokana na mvua ambazo zinaendelea kunyesha.

" Kwa sasa tumerudi tupo sehemu ya ujenzi ila kwa sasa tutaondoa mawe kwa ajili ya  greda liweze kusafisha na tupange mawe tena upya na kifusi ili kuwapunguzia adha ya usumbufu wananchi kuhusu barabara hii." Amesema Mnyambogwe

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: