Bima ya afya ni nini?

Bima ya afya ni mfumo wa kujiunga kwa hiari ama kwa lazima unaomhakikishia mwanachama kugharamiwa gharama zinazojitokeza katika kupata huduma za kiafya zikiwemo kumwona daktari, kufanya vipimo pamoja na kupata matibabu na dawa kwa mwanachama husika.


Bima ya afya ni kama mkataba unaoingiwa na anayetaka huduma pamoja na mtoa huduma kwa kupitia mifuko au taasisi inayowaunganisha mtoa huduma pamoja na mhitaji wa huduma husika.

Mara nyingi Bima ya afya hujumuishwa kwenye makato anayoyatoa mwajiri kwa waajiriwa wake katika kufanya malipo.


Pia zipo bima zinazowahusu watu binafsi, wazee na wasiojiweza, wajawazito na wengine wenye mahitaji maalumu bila kusahau wanafunzi kipindi cha masomo yao.

UMUHIMU WA BIMA YA AFYA.

1.Kutibiwa kwenye vituo zaidi ya 9,000 kuanzia ngazi ya zahanati,hadi Hospital za Rufaa za Taifa vikiwemo vya Serikali,Mashirika ya dini na binafsi.

2. Uhakika wa Matibabu wa Mume,Mke,Watoto,na wazazi wote hata kama huna fedha.

3.Kupata matibabu ya msingi na ya Kibingwa.

4.Kupata dawa zote kulingana na ushauri wa Daktari.

5.Kupata vipimo vikubwa na vidogo.

6.Kupata huduma za meno na macho.

7.Hakuna mipaka unaweza kutibiwa Mkoa wowote Tanzania Bara na Zanzibar

Share To:

Post A Comment: