Mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy akiongea na viongozi mbalimbali na wadau wa maendeleo wilaya ya Iringa wakati akihamasisha zoezi la utanzaji wa mazingira katika wilaya hiyoMtendaji wa kata ya Ilolo Mpya akifaatilia maagizo ya mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy juu ya utunzaji wa mazingira na usafi wa mazingira.

Emmanuel Ngabuji afisa Tarafa, Tarafa ya Pawaga akifaatilia maagizo ya mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy juu ya utunzaji wa mazingira na usafi wa mazingira

Na Fredy Mgunda, Iringa

Mkuu wa wilaya ya Iringa ametoa miezi mitatu kwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Iringa kuhakikisha wanapanda miti KANDOKANDO ya barabara zote kuu ili kutunza mazingira.


Akizungumza wakati makadirio ya bajeti ya Halmashauri hizo, mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy aliwataka maafisa mazingira kuhakikisha wanapanda miti mingi kila eneo kwa lengo la kutunza mazingira na kuupendezesha mji.

Kessy alisema kuwa lazima miti ipandwe kwenye barabara zinazoingia na kutoka katika wilaya hiyo ili kuweka mazingira yakuvutia wageni wanaoingia na kutoka katika barabara zote za wilaya ya Iringa.

Alisema kuwa kila mtendaji wa mtaa, Kijiji na kata wahakikishe wanasimamia vilivyo zoezi la upandaji miti katika maeneo yote yanayohitajika kupandwa miti.

Lakini pia aliwataka viongozi wa Halmashauri hizo kuwakamata watu wote wanaotupata takataka hovyo na kuwalipisha faini bila woga ili kuweka mazingira Safi ya wilaya ya Iringa kama ilivyokuwa na sifa hizo kila Mara.

"Kamateni watu wote wanaotupata takataka hovyo iwe kwenye gari au anatembea kwa miguu kamateni bila woga na mimi nitawatumia picha kila mara nitakapo muona mtu anatupa taka hovyo,Mimi ni mwanamazingira hivyo mazingira ya Iringa lazima yawe Safi muda wote" alisema Kessy

Kwa upande wake afisa mazingira wa Manispaa ya Iringa Getruda Maxwell alimhakikishia mkuu wa wilaya kutekeleza agizo hilo ndani ya miezi mitatu kwa suala hilo lipo kwenye mipango ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Maxwell alisema kuwa zoezi hilo litakamilika kwa asilimia 100 kwa kuwa walishalipangia bajeti ya upandaji miti katika Halmashauri hiyo.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: