Na John Walter-Manyara.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere amewataka wanufaika wa Pesa za TASAF kuzitumia vyema kwa kujiletea maendeleo ili kuepuka kuwa wategemezi.

Nyerere ametoa wito huo wakati akizungumza na walengwa katika kata ya Nangara ambayo ni mongoni mwa kata nane  za mji wa Babati yenye mitaa saba ambapo jumla ya walengwa 244 wamepekewa shilingi Milioni 10,646,000.

Katibu tawala mkoa wa Manyara Karolina Mthapula amewaambia wanufaika hao kuwa endapo fedha hizo watazitumia vyema kwa lengo kusudiwa wataweza kubadilisha maisha yao.

Halmashauri ya mji wa Babati ina jumla ya kata 8 zenye mitaa 35 na vijiji 13 ambavyo vote vinanufaika na mradi wa uhaulishaji wa fedha kwa kaya masikini huku kukiwa na jumla ya kaya za walengwa 2325 ambapo wamepatiwa kiasi cha silingi 97,894,327.

Mratibu wa TASAF mkoa wa Manyara Rashid Shedafa amesema kati ya walengwa hao 1130 wanapokea fedha Taslimu na walengwa 1195 wanapokea kwa njia ya mtandao (simu za mkononi).

Amesema changamoto iliyopo ni baadhi ya walengwa kutumia fedha zinazotolea katika matumizi yasiyostahili kama ulevi, kufanya sherehe badala ya kutumia katika kuanzisha biashara ndogondogo ambazo zingeweza kuwasaidia  baadaye.

Nao wananchi walionufaika na Mpango huo wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuonesha nia ya dhati kuwasaidia watu/kaya masikini kwa kuwapatia fedha zitakazowawezesha kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kuahidi kuzitumia kama ilivyokusudiwa.


Share To:

Post A Comment: