Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa hakuna mwanafunzi atakayekosa nafasi ya kusoma kutokana na changamoto ya ukosefu wa madarasa.

Kupitia taarifa yake fupi kwenye mtandao wa ‘Twitter’ , Rais Samia amesema katika siku 100 zilizopita serikali imefanikiwa kujenga madarasa ya sekondari 8,000 pamoja na samani zake nchi nzima ambayo yataanza kutumika wiki ijayo.

“Hatua hii ya kihistoria ni ukombozi kwa wanafunzi zaidi ya 400,000,” amesema Rais Samia.

Share To:

Post A Comment: