Watu wengi wanapenda kupendezesha nyumba zao ama ofisi kwa mapambo mbalimbali ikiwemo maua.

Ama kwa hakika, bustani za maua mbalimbali zinazotunzwa vizuri ni kivutio kikubwa husasani majumbani na sehemu zingine mbalimbali.

Vijana wengi wameanzisha biashara ya kuuza maua na wengine wakifanya kazi ya kutengeneza bustani (garden) kwa utaalamu.

Biashara hii ambayo inakua kwa kasi imeweza kuwakwamua kiuchumi kwa kuwapatia kipato.

Ukipita sehemu mbalimbali kando kando mwa barabara utaona bustani nzuri zilizopambwa kwa maua pamoja na mapambo mengine ikiwemo ukoka, makopo na vyungu vilivyotengenezwa kwa umaridadi kabisa vikingoja wateja tayari kwa kuuzwa.

Raheli Massawe ni mfanya biashara wa maua mkoani Kagera.

Anauza maua na makopo ya kupandia maua. Anasema “nilianza biashara ya kuuza maua mwaka juzi, mimi napenda sana maua, nilianza kwa kupand anyumbani kwangu, watu wakayapenda ndipo nikaanza kuyauza.”

Raheli anasema biashara hiyo imekua ikikua siku hadi siku, watu mbalimbali wakifika nyumbani kwake wanavutiwa na maua na huwauzia.

“Nilipoanza nilikuwa nikiwauzia maua pekee, lakini sasa nauza na makopo ya kupandia maua. Huwa ninaagiza makopo kutoka Dar es Salaam na kuyauza Bukoba. Biashara hii ni nzuri, haichukui muda wangu mwingi.” Anasema.

Ametoa wito kwa vijana kuacha wasio na ajira kujiajiri kwa kuwa wabunifu na kufanya biashara zitakazo wakwamua kiuchumi.

“Kwa sasa ajira ni ngumu sana, vijana wengi wamehitimu lakini hawana kazi za kufanya, vijana wengi wanashindwa kujiajiri kutokana na changamoto ya mitaji, kuna biashara ambazo haziitaji mitaji mikubwa kama hii ya maua, nawasihi vijana wajitume na kuanzisha biashara ndogo ndogo kuliko kutegemea kuajiriwa pekee.” amesema Rahel.

Share To:

Post A Comment: