Na John Walter-Mbulu

Baraza la madiwani halmhauri ya mji wa Mbulu Mkoani Manyara limeketi na kujadili matumizi ya halmashauri na kupitisha bajeti ya zaidi ya shilingi billioni 24 kwa mwaka 2023-2024.

 

Bajeti hiyo imepitishwa baada ya kikao kilichoketi siku mbili kwa ajili ya kujadili mapato na matumizi ya halmashauri hiyo.

 

Akitangaza kupitishwa kwa bajeti hiyo , mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa mbulu Yefred Muyenzi amelishukuru baraza kwa kupitisha bajeti hiyo.

 

Aidha Mkurugenzi Muyenzi , amewataka wakuu wa idara kusimamia fedha hizo zitumike kama zilivyoidhinishwa na baraza.


Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Mbulu Bi Sara Sanga, ametumia kikao hicho cha baraza la madiwani kutoa wito kwa wazazi na walezi wa kuhakikisha wanafuzni wote wenye sifa za kwenda shule wanapata haki hiyo.

 

Aidha amewataka wazazi kuhakikisha wanachangia gharama za chakula kwa watoto wao ili kuwawezesha kusoma kwa utulivu.

Share To:

Post A Comment: