Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa kupitia jumuiya ya wazazi George Gandye akiongea na wazazi juu ya umuhimu wa kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa watoto na jamii kwa ujumla ili kuwa na kizazi bora



Na Fredy Mgunda, Iringa.


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia jumuiya ya wazazi George Gandye amewataka wazazi kushiriki katika vita ya vitendo vya ulawiti na ushoga vinavyoanza kuonekana vya kawaida kwa baadhi ya jamii za kitanzania.

Gandye alisema kuwa kuanza kushamili kwa vitendo vya ubakaji, ulawiti na ushoka ni dalili mbaya za malezi kutoka kwa wazazi hivyo wazazi wanatakiwa kurudi kwenye misingi ya kuimarisha maadili ya familia.

Alisema kuwa msingi wa kuporomoka kwa maadili watoto wa kinzania ni kutoka kuharibika kwa maadili ya wazazi hivyo jumuiya ya wazazi ya chama cha mapinduzi inajukumu kubwa la kuielimisha jamii irudi kwenye misingi inavyotakiwa.

Akitoa nasaha zake katika kikao cha Baraza Kuu la Jumuiya ya mkoa huo kilichofanyika leo mjini Iringa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia jumuiya hiyo George Gandye alisema; "Vitendo hivi ni moja ya changamoto zinazotakiwa kushughulikiwa na jumuiya yetu."

Aliwataka wanaume wa Iringa kukumbuka historia ya ujasiri wao na kuwa wa kwanza kuonesha kwa vitendo kutokubaliana na vitendo hivyo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Iringa, Fadhili Ngajilo alisema jumuiya yake imepanga kusaidia kutoa elimu ya afya ya uzazi ili kuokoa kizazi cha sasa na kijacho kutokana na kuongezeka kwa vitendo hivyo.

Mbali na vitendo hivyo kukatazwa kwa mujibu wa sheria na maandiko matakatifu ya dini mbalimbali, alisema vina fedheha kwa jamii na moja ya sababu ya kukatisha ndoto za kimaisha za baadhi ya watu hususani watoto.

Ngajilo alisema wana kazi kubwa ya kufanya ili kuilinda jamii wakiwemo watoto hao dhidi ya ukatili wa kijinsia na mmomonyoko wa maadili na akaitaka jumuiya hiyo kubeba dhamana hiyo kwani ni moja ya wajibu wake.

Katika kikao hicho ambacho pia kilitumika kutoa semina ya uongozi kwa viongozi wa jumuiya hiyo wa kutoka wilaya zote za mkoa wa Iringa, Ngajilo alizungumzia ruhusa ya mikutano ya hadhara akisema ni wajibu kwa kila mwana CCM  kufungua masikio yake na kusaidia kutoa ufafanuzi wa yale yatakayokuwa yanazungumzwa na wapinzani wao.

"Kazi ya kujibu hoja za wapinzani isiachwe kwa viongozi tu. Wanachama nanyi mna nafasi yenu, angalieni nini kimefanywa na kinaendelea kufanywa katika maeneo yetu, saidieni kuwaeleza wananchi," alisema

Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa, Aggrey Tonga alisema jumuiya ya wazazi ina kazi kubwa ya kusaidia kuirudisha jamii ya watanzania kwenye maadili ambayo kuporomoka kwake kumechochea kuibuka kwa vitendo hivyo vya ulawati na ushoga.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, ubakaji, ulawiti na kufanya mapenzi 'kinyume na maumbile' ni baadhi ya makosa ya jinai ambayo mtu akikutwa na hatia adhabu yake ni pamoja na kifungo jela.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: