Na John Walter-Karatu

Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Mangola Juu Kata Ya Daa

wilayani Karatu mkoani Arusha amefariki dunia baada ya

kushambuliwa na mbogo.

Tukio hilo limetokea tarehe 23 Januari mwaka huu wakati mwanamke huyo

aitwaye Katarina Ngaida akimsindikiza mtoto wake shule.

Akielezea kuhusu tukio hilo diwani wa kata ya Daa,  Alex Martin

Sidawe amesema mama huyo alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa

hospitalini.

Kufuatia tukio hilo diwani wa kata hiyo ameiomba serikali

kufungua shule mbili mpya ambazo zimejengwa ili kuwaondolea

adha wazazi ya kuwasindikiza watoto kwa kuwa shule ziko mbali.

Share To:

Post A Comment: