Kijana James Yustar akifanya mahojiano na mwandishi wa habari  juu ya historia yake ya Maisha yaliyompelekea kuwa mtoto wa mtaani.


Na Denis Chambi, Tanga.

 Watoto wa mtaani ni moja ya kundi la watoto ambao wengi ni wahanga wa vitendo vya ukatili vinavyotekelezwa kila kukicha wa wazazi , walezi na hata watu wa karibu wengi wao wakitupwa jalalani na sehemu ambazo sio salama kwa afya na maisha yao kwa kile kinachiodaiwa kuwa ni hali duni ya maisha katika familiya wanazotokea. 

Wazazi kushindwa kutekeleza majukumu yao ya malezi ipasavyo na hatimaye kutelekeza na kuzikimbia familiya zao huku kwa asilimia kubwa wanawake wakiachiwa jukumu la malezi ambapo hata hivyo wanashindwa kuyamudu maisha. 

Hali hii imemkuta kijana James mwaka 1994 mkoani Arusha wakati akiwa na umri wa mwaka mmoja alitupwa jalalani na mama yake mzazi na hatimaye kukimbia kusiko julikana mpaka sasa hajulikani alipo ,kwa bahati nasibu James akiwa jalalani amefungwa kwenye boksi Mtawa wa kike aliyefahamika kwa jina la Yustar Justine Ebrania akiwa anapita karibu na maeneo hayo anamuona Mbwa akiwa amebeba boksi mdomoni mwake akiwa anajitafutia riziki yake. Sister Yustar anaamua kumkimbilia Mbwa bila ya kujua kilichomo ndani ya boksi anafanikiwa kulichukuwa na analifungua ndani anaona kitoto kichanga ambaye ni James .

 Sister(Mtawa) anaamua kumuokoa James na kwenda kuishi naye nyumani kama mwanae akimlea katika makuzi ya kimwili na kiroho na hapo ndio historia ya maisha ya mtoto James yanaanza na anapewa jina la pili la Mtawa yule ambapo sasa anaitwa James Yustar. Mwaka 1997 James akiwa darasa la pili na umri wa miaka 7 ilikuwa ni tarehe 25 mwezi wa 5 wakiwa wanasherehekea siku ya kuzaliwa kwa kijana yule wakati wanarudi nyumbani wakiwa kwenye gari njiani katika maeneo ya UNGA LIMITED Arusha aligundua mama yake kila inapofika tarehe hiyo Mtawa yule anakuwa hana furaha aliamua kumuuliza kiundani kutaka kujua nini hasa kinachomsumbua mama yake lakini ukweli ni kwamba hakuwa mama yake aliyemzaa na ndio chanzo cha Mtawa yule kuwa katika hali ile kila mwaka inapofika siku hiyo. 

Sister( Mtawa Yustar) aliamua kumweleza ukweli James na kuwambia kuwa anaishi naye tu lakini hamjui baba wala mama yake mzazi mara baada ya kumuokota jalalani aliendelea kumlea na kuhakikisha anapata malezi na haki zote zimpasazo mtoto ikiwa ni pamoja na elimu. Mara baada ya James kuelezwa kinang'aubaga juu ya maisha yake yalivyokuwa baada ya kuokotwa jalalani waliendelea kuishi pamoja kwa mani furaha na upendo mkubwa .Mama yake James alikuwa anamiliki maduka mawili ya dawa yaliyokuwa Moshi na Arusha mjini na pia anaendelea na ujenzi wa Zahanati , Hostel ya kuhifadhia watoto wa mtaani na wanawake wasiojiweza maeneo ya Mianzini mkoani humo. 


Wakati Mama yake James anatoka kuangalia maduka yake alipata ajali ya gari na kuumia maeneo ya kifua na kupelekwa hospital hivyo kupelekwa Afrika Kusini kwaajili ya matibabu zaidi akikaa kwa wiki mbili na hatimaye kuruhusiwa kurudi nyumbani Tanzania , siku chache baada ya mama kurudi alimuita James na kumkabidhi hati tatu za nyumba , na kiwanja , kadi ya benki na kisha albamu ya picha . James alivipokea vitu hivyo kwa mikono miwili licha ya kujiuliza ni kwanini mama yake alimkabidhi vitu vyote hivyo ambayo vilikuwa vikisimamiwa na mjomba wake aliyekuwa akiitwa Mayasa Mbusia. 

Hazikupita siku nyingi sana mama yake James alizidiwa tena na maradhi na kukimbizwa hospital na mjomba Mayasa lakini hata hivyo umauti ulimkuta akiwa njiani mwaka 1997 , James hakuweza kushiriki mazishi ya mama yake kutokana na tatizo lilomkuta likampelekea kupoteza fahamu kila mara hivyo akafungiwa nani ya chumba huku akiwa chini ya uangalizi mkali. 

Baada ya msiba wa mama yake James matatizo yakaanza kuikumba nyumba ile, mjomba Mayasa akaanza kuwafukuza wafanyakazi wote waliokuwa wakifanya kazi katika maduka kumfuata James kumlazimisha ampatie hati za nyumba ambazo alipewa na mama yake ili akachukue mkopo naye alikubali . Siku moja James akiwa Shuleni alifuatwa na watu asiowajua wakiwa wanaendesha gari la mjomba wake , aliondoka na kwenda kuingia ndani ya gari licha ya kuwa hakumuona mjomba baada ya kuwauluiza waliokuwa ndani ya gari walimjibu kuwa amewatuma waende kumchukuwa ili akamuone jomba wake aambaye alipata ajali. 


Ghafla alianza kushikiliwa na kujazwa matamba na sponji mdomoni ili asiweze kutoa sauti huku akifungwa kamba mikono na miguu gari ikawa inaendeshwa kwa kasi . Baada ya umbali mrefu walienda kumshusha James katika mazingira asiyoyajua huku mvua kubwa iliyokuwa imeambatana na radi ikiwa inanyesha akaja mtu na kumfunga kitambaa kizito usoni .

 Mara ilipiga tena radi kubwa na tetemeko kubwa likakumba eneo lile James akasikia vilio na makelele vya watu wale ambao waliangukiwa na mti mkubwa , ndipo akapata wazo la kuondoka maeneo yale akawa anatambaa kwa kutumia makalio yake akaanza kusota usiku kucha akiwa anaugulia maumivu makali yaliyosababishwa na matambara na sponji aliyokuwa amejazwa mdomoni akiwa anaendelea mbele bila ya kujua aendako alikutana na wanyama wengi wakubwa kwa wadogo lakini hakuna aliyewahi kumdhuru zaidi akitetemeka kwa baridi kali kwa siku tatu akiwa anaendelea na safari yake aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu alipokuja kuzinduka alijikuta katikati ya jamii ya watu wa Kimasai wakampepeta na kumkandakanda . 

Baanda ya wiki moja james alipata nguvu ila akawa hawezi kuongea zaidi akitumia kuongea kwa ishara na kuandika chini kwa bahati mbaye wale wamasai walikuwa hawajui kusoma wala kuandika. Baadaye James alipona kabisa ila akawa hawezi kuongea kabisa akawa ni bubu, akaanza kuishi katikati ya jamii ya kimasai James anasema "siku moja tukiiwa tumeenda kuchunga Ng'ombe walinipeleka hadi mahali waliponiokota , niliumia na kulia sana siku ile maana katika maisha yangu sikujua kama nitapita katika maisha yale niliyoishi , nilitamani siku moja sauti yangu itoke niwape asante , waliendelea kunielekeza kuwa waliniokota nikiwa nimevaa sare za shule nilizidi kuumia waliponiambia kuwa siku ile ilikuwa siku ya mwishio kama nisingezinduka wangeniacha pale na wao wangehamia sehemu nyingine". 

"Nilikuwa naumia sana moyoni kila nilipofikiria juu ya maisha yangu, wakati mwingine nilikuwa nafikiri kuwa nipo katika ndoto na asubuhi nitaamka. Nikiwa nimeishi na wale wamasai kwa muda wa mwaka mmoja wakati huo nilianza kuongea kidogo kidogo hivyo niliomba niweze kurejea nyumbani Arusha. Nakumbuka huo ulikuwa ni mwaka 1999 wamasai waliniruhusu kuondoka wakanizawadia Ng'ombe wawili wakanisindikiza katika gari lililokuwa likikokotwa na Punda mpaka Manyara katika mnada ,tuliuza kila Ng'ombe kwa laki moja moja nikapata nauli nikarejea Arusha." 

"Niipokuwa Arusha nilianza kupita katika maduka yetu lakini sikuona hata duka moja likiwa wazi yote yalibadilishwa majina na kuuzwa bidhaa zingine , nakumbuka wakati huo nilikuwa na umri wa miaka nane niliamua kunyoosha hadi nyumbani nilipofika kuna mabadiliko makubwa sana pale nyumbani na kwa kuwa nilikuiwa nimevaa nguo za kimasai hakuna mtu aliye kuwa akinijua nilipotaka kuingia ndani walinzi walinikataza walianza kuniuliza maswali mengi lakini hatukuweza kuelewana mara lilikaja gari na kuingia akiwemo mzungu wa kiume na mama mmoja wa kiafrika walinzi wakaniambia hawa ndio wenye hii nyumba , kisha wakaniuliza unasema ni nyumba yenu baba yako anaweza kujenga nyumba kama hii" James anasiumulia.

"Nilishindwa kuvumilia nilianza kulia , nililia sana mpaka wale walinzi walianza kunifukuza niliondoka na kuzunguka nyuma ya nyumba ambako kulikuwa na mti mdogo wa Mnazi ambako ndipo tulipomzika mama na hata kabuli la mama lilikuwa halipo wakati tulikuwa tumelijenga kwa tiles uchungu ulinishika nikajikuta nalia kwa sauti mpaka nikawastua watu wengine walinzi wakaja kunifukuza tena lakini nilikuwa nazunguka maeneo yale yale, siku ile nilizunguka mpaka usiku lakini sikumuoana anko , usiku ulipokuwa mkubwa niliamua kupanda juu ya mti wa muembe na kulala wiki nzima na kwa kuwa nilikuwa na pesa asubuhi niliamua kwenda kununua nguo na kuvaaa bila kuoga na yale mashuka ya kimasai niliyatupa"

"Nilipokuwa kule mjini nilikutana na Bruno anauza sigara nilishangaa sana yupo katika hali ile maana tulikutana muda mrefu wakati mimi na mama tulipokuwa tunatembelea watoto yatima kule Unga limited, Bruno yeye alinieleza matatizo yake baada ya mama yake kufariki na baba yake kumuoa mke mwingine aliyemchukia hali iliyompelekea baba yake kumtoa nyumbani na kumpeleka katika kituo cha kulea watoto yatima"

Maisha ya James yakaanza upya akiwa anaishi na kuranda randa mtaani yeye pamoja na rafiki yake Bruno wa siku nyingi aliyezoea masiha ya mtaani akivuta sigara bangi na kunywa pombe wakakukutana na changamoto za kila aina wakiwa mtaani ikiwa ni pamoja na kuvamiwa na majambazi, kupelekwa polis wakipgwa kwa kudhaniwa kuwani wezi . James na Bruno waliishi mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es salaam, Arusha Mbeya kote huko wakijitafutia riziki zao za kila siku kama watoto wa mtaani.

 Katika mahojiano aliyoyafanya na muandishi wa makala hii James Yustar amesema kuwa kuna mtazamo hasi kwa jamii juu ya wimbi la watoto wa mtaani wengi wakionekana kuwa hawahafai kuchangamana na watu wengine wakiishia kunyanyapaliwa kutengwa lakini kwa upande wake anaamini kila mtu alieletwa katika uso wa dunia hii wakati anayo haki ya kuishi kupendwa na kila mmoja na yupo kwa makusudi maalum. 

" Katika jamii yetu bado kuna unyanyapaa , kutengwa na hiyo yote ni kutokana na udumavu wa fikra na watoto wa mtaani wanazalishwa na jamii hiyo hiyo lakini sisi tunawahukumu kuwa ni watoto wa baya wakati jamii yenyewe ndi chanzo cha hawa watoto, fikra mgando ama fikra dumavu ni tatizo kubwa sana kwa jamii zetu ambazo zinapelekea kupoteza kizazi ambacho kinaweza kuja kutatua sehemu ya changamoto na kusaidia pia kuleta maendeleo. 

Kufwatia maisha aliyopitia James na misukosuko aliyoishi tangu akiwa mdogo sasa ameanzisha taasisi ya JAMES FOUNDATION ambayo ipo mahususi kwaajili ya kupambana na wimbi la watoto wa mtaani wakiwashauri kuondokana na hali hiyo na hatimaye kuwarudisha kwenye jamii waendelee na shughuli zao za kujipatia kipato na hatimaye kuchangia maendeleo ya Taifa 

"Leo hii mimi ni kijana nieamnzisha taasisi yangu ya kijamii ili iwahudumuie wale vijana wenzangu ambao ni wahanga halisi wa maisha ya ukatili hasa watoto wa mtaani , mimi ninaamini kila kiumbe anayezaliwa hapa duniani hasa binadamu anazaliwa ili aje kutatua changamoto zilizopo katika jamii yake " Kipo kitabu chenye historia ya maisha yoteya James Yustar. 

Kwa mawasiliao zaidi juu ya historia hii 

 James Yustar-(Mhusika wa historia hii-0657-579-300) 

Denis Chambi- (Mwandishi wa habari hii 0653-852-474/0628-651-395). 
Share To:

Post A Comment: