Mbunge wa Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu leo tarehe 05/01/2023 amefanya ziara katika kata ya Chongoleani lengo likiwa ni kakagua shughuli za maendeleo na kupokea kero za wananchi.


Katika ziara hiyo, Mhe Ummy alikutana na viongozi wa kamati ya maendeleo ya kata na kupokea taarifa ya Maendeleo ya Kata kabla ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ktk kata hiyo.

Kata ya Chongoleani kwa mwaka wa fedha 2022/23 wamepokea fedha za ujenzi wa Hosteli ya Shule ya Sekondari Ndaoya sh. Milioni 45 na shilingi Milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Walimu. Pia wamepokea shilingi milioni 90 za ujenzi wa maabara Sekondari Ndaoya na shilingi milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa Darasa Sekondari ya Chongoleani.

Baada ya kupokea taarifa hiyo, Mhe Ummy aliambatana na diwani wa Chongoleani Mhe Mwaveso Mbega, Mchumi wa Jiji, Mwakilishi wa TANESCO, wajumbe wa kamati ya siasa ya kata, Mtendaji Kata na Viongozi wa mitaa yote 4 ya kata ya Chongoleani kuangalia miradi ya maendeleo ikiwemo eneo la ujenzi wa wodi ya kujifungulia ktk zahanati ya Chongoleani na pia kukagua ujenzi wa darasa Shule ya sekondari Chongoleani.

Pia Mhe Ummy ametembelea eneo la Bagamoyo kuona utekelezaji wa ahadi zake alizozitoa yeye na Diwani kuhusu kutatua kero ya maji na barabara ktk eneo hilo ambazo zimetekelezwa kwa ufanisi.

Aidha Mh Ummy ametembelea Mtaa wa Putin kuona utekelezaji wa mradi wa uwanja wa mpira na eneo lililotengwa kujenga zahanati mtaa wa Ndaoya na kumalizia ziara yake eneo la Helani ambalo kuna mradi wa usambazaji umeme wa bei nafuu chini ya TANESCO/REA sambamba na kuona utekelezaji wa mradi wa maji ktk Mtaa huo.

Mhe Ummy amewahakikishia wanaChongoleani kuwa licha ya maji kufika na barabara nyingi kuchongwa ktk kata hiyo bado ataendelea kushirikiana na Diwani na Wenyeviti wa Mitaa kutatua kero zilizobaki.

Aidha Mhe Ummy ametoa wito kwa wazazi/walezi wenye watoto wa umri wa kuanza elimu ya Awali na Msingi kuwaandikisha watoto wao shuleni kwani hadi sasa uandikishaji sio wa kuridhisha.
Share To:

Post A Comment: