Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Morogoro ikiongozwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Albert Msando ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo inalazimika kuwakamata  watu 12 waliovamia  katika eneo la mwekezaji na kuharibu mazao na vitu mbalimbali ikiwemo kung'oa zao la.katani 


Kitendo cha uvamizi wa wananchi hao katika eneo Hilo Kimetafsiriwa kama uvunjifu wa amani  kwani tayar mwekezaji huyo alishatoa  ekari 4,500 kati ya ekari  elfu kumi na Mia  sita anazomiliki kihalali na kulitoa Kwa serikali ili kupanga shughuli mbali mbali ikiwemo makazi lakini bado wameendelea kuvamiwa eneo lilolobaki na kuanzia kulima

DC Msando alisema siku za hivi karibuni mkuu wa mkoa Morogoro Fatma Mwassa alifika katika eneo Hilo na kuwataka wananchi kuacha kufanya shughuli zozote na kusubr zoezi la uhakiki lakini siku chache badae watu wengine wamevamia shamba la mwekezaji na kufanya uharibifu nje ya eneo alilotoa serikalini kisha kugawana  Kwa ajili ya viwanja na Kilimo kinyume na utaratibu.


Share To:

Post A Comment: