Baadhi ya Wakaguzi wa halmashauri zote saba mkoani Manyara walio chini ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) wamesema hakuna njia nyingine ya kuboresha huduma ya Uboreshaji wa utoaji wa huduma kwenye maduka ya dawa muhimu na mifugo kama jitihada za kuwaondoa wahudumu wasiokuwa na sifa hazitachukuliwa kwa uzito unaostahili.


Kauli hiyo wameitoa  baada ya TMDA Kanda ya Kaskazini kuendesha mafunzo ya siku moja ya kuimarisha ukaguzi,mbinu za ukaguzi kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu zilizopo kwenye sheria ya dawa sura ya 219 yaliyowashirikisha wafamasia,wataalam wa maabara na maafisa ugani wa mifugo wa halmashauri hizo yaliyofanyika mjini Babati.

“Nimewezeshwa mbinu za ukaguzi na kutambulika,lakini kuna changamoto nyingi kwenye ukaguzi baadhi ya watoa huduma hawana sifa,utitiri wa maduka yanayoanzishwa pasipo kufuata utaratibu mbali ya uhaba wa wakaguzi lakini pia tunashindwa kuyafikia” anaeleza Rodgers msechu mmoja wa wakaguzi wapya.

Aidha Msechu amesema ili kufanikisha malengo ya kuboresha utoaji wa huduma TMDA na halmashauri zinapaswa kujipanga ili kuhakikisha wakaguzi wanafika katika ameneo yenye mazingira magumu kijiografia sambamba na kuongeza wakaguzi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu katibu tawala Halphan Omaary alisema ni vyema kila mkaguzi akafanya kazi kwa kuzingatia sheria  huku akisisitiza kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza  kufikia malengo ya kulinda afya ya jamii.

Awali akitoa mafunzo hayo afisa mwezeshaji TMDA Kanda kaskazini Dr.Elifuraha nyunza amewataka wakaguzi hao wapya na wazoefu kutumia stadi za ukaguzi sambamba na kufuata taratibu,kanuni na sheria za ukaguzi na kuvumilia kauli zisizo na staha.

"Wakaguzi mnatakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuacha tabia za vitisho kwa wafanyabiashara wa madawa mkiwa kazini kwani hali hiyo inajenga lawama kwa halmashauri zenu".

Nae  Mwakilishi wa  meneja wa TMDA Kanda ya Kaskazini na Mkaguzi  Elia Nyaura anakiri kuwepo kwa uhaba wa wakaguzi lakini pia akisisitiza wakaguzi wapya kuzingatia sheria ya dawa sura 219 na ukaguzi unaokubalika kwa mujibu wa sheria.

Nyaura alisema kwasasa TMDA,TAMISEMI pamoja na halmashauri wameamua kushirikiana Ili kusaidia kufuatilia taarifa za madhara ya dawa na vifaa tiba,kusimamia kuharibu bidhaa zisizofaa,kutoa elimu kwa umma,kuchukua hatua za kisheria pamoja na kuhakiki vibali vya biashara hizo kama ni hali.

"Lengo kuu la ushirikiano kati ya TMDA,TAMISEMI na halmashauri ni kuboresha utendaji kazi na kutoa huduma kwa wananchi kwa karibu na kwa wakati na hatimae kulinda afya ya jamii kwa kuthibiti ubora, usalama na ufanisi wa dawa na vifaa tiba"alisema Nyaura.

Nyaura alisema faida za ushirikiano huo ni kuwa na mtandao nchi nzima katika shughuli za uthibiti ubora na usalama wa bidhaa ikiwa ni pamoja na kuwatumia wakaguzi waliochini ya TAMISEMI katika shughuli za udhibiti wa bidhaa ili kulinda afya ya mtumiaji.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr. Damas Kayera amesema ili mwananchi aweze kuwa na afya bora sehemu ya dawa,vifaa tiba na vitendanishi lazima kuwa  bora.

“Tunapozungumzia ubora tunataka vifaa hivyo viwe salama na visilete madhara bali ufanisi ili kufikia malengo hayo lazima wawepo wakaguzi wanaosimamia na wenye weledi”

Hata hivyo baadhi ya wananchi mjini babati licha ya kuishukuru TMDA kufanya ukaguzi huo,lakini wameiomba serkali kuyafunga maduka yenye watoa huduma wasio na sifa na kuwapa elimu zaidi.


"Kwanza tukubali maduka mengi yanayotoa huduma hizi yanamilikiwa na wastaafu haohao waliotoka serikalini,wanasimama kama kivuli tu lakini badala yake wanawatumia watoa huduma kwa kuwaandikia dozi kwenye vikaratasi hii ni hatari” alisema Hussein sherifu mkazi wa Babati.

Share To:

Post A Comment: