Na Mario Mgimba;Njombe


Mkazi wa Ludewa Kijijini Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Baraka Alphonce (20), anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumkata kiganja cha mkono wa kushoto Boss wake aliyekuwa akimdai Tsh Elfu 65 alizolima kwa kutumia ng’ombe.


Kwa mujibu wa Patrick Mdege (35) aliyejeruhiwa na Mtuhumiwa huyo anasema Kijana huyo alikuwa ni Mfanyakazi wake lakini amemgeuka na kumkata kiganja chake mara baada ya kutokea ugomvi baina yao.


“Alikuwa amefanya kibarua kwa Mtu cha kulima kwa kutumia ng’ombe wangu wanaotumika kulimia, aliyemlimia akaja kusema ile hela imetoka na Mimi nilimzuia asimpe ile hela bila Mimi kuwepo, nilipomfuata yule Dogo akaanza kunitukana nikamwambia Dogo uwe na busara nimekulea kwa muda mrefu nikampiga kofi kumbe kwenye jembe la ng’ombe kulikuwa na panga akachomoa sasa Mimi ile ni panchi likafika mkononi”


RPC wa Njombe Hamis Issah amesema kiganja hicho kilianguka ardhini na kuokotwa wakati majeruhi akikimbiakimbia, na alipofikishwa Hospitali kiganja hakikuweza kuunganishwa lakini hata hivyo Mtuhumiwa yuko mikononi mwa Polisi akisubiri kufikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.


Aidha Kamanda  Issah amewaonya wananchi kutojichukulia sheria mkononi pasipo kufuata taratibu zinazotakiwa na mamlaka husika.

Share To:

Post A Comment: