Askofu Mkuu wa Kanisa la ABC Tanzania lililopo Mtaa wa Mandela jijini Dar es Salaam, Flaston Ndabila (kushoto)) akizungumza na wajane na wagane wakati wa hafla ya kukabidhi  msaada wa chakula (mchele) nguo na fedha iliyofanyika leo Desemba 26, 2022.

Mjumbe wa Serikali ya mtaa wa Mandela, Tabrisa Bushiri akitoa neno la shukurani.
Mke wa Askofu Ndabila, Janeth Ndabila  akitoa nguo katika hafla hiyo.
Mke wa Askofu Ndabila, Janeth Ndabila akitoa msaada wa nguo katika hafla hiyo.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo Juma Hassan akizungumza.
Wajane wakiwa kwenye hafla hiyo.
Hafla ikiendelea.
Mchele ukiwa kwenye mifuko tayari kwa kugaiwa walengwa.
 Nguo za aina mbalimbalizilizotolewa kwa walengwa.

Picha ya pamoja baada ya kutolewa kwa msaada huo.

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam. 

KANISA la Abundant Blessing Church (ABC) lililopo Mtaa wa Mandela jijini Dar es Salaam limetoa msaada wa chakula, nguo za aina mbalimbali, viatu na fedha kwa ajili ya kuwasaidia Wagane na Wajane 40 wanaoishi kwenye mtaa huo..

Akizungumza  wakati wa kukabidhi msaada huo Askofu mkuu wa kanisa hilo hapa nchini, Flaston  Ndabila alisema wamekuwa wakiguswa na changamoto mbalimbali za Wajane na wagane na makundi mengine yanayoishi jirani na kanisa hilo na maeneo mengine ya jirani na kuwa  wameweka utaratibu kila mwaka kutoa msaada huo.

"Huu ni mwaka wetu wa sita tumekuwa tukifanya hivi  hasa kipindi hiki cha Sikukuu za mwishoni mwa mwaka za Krismas na mwaka mpya na leo tumetoa msaada huu ikiwa ni kuadhimisha siku ya kupeana zawadi baada ya krismas (Boxing day) alisema Ndabila.

Ndabila alisema kutoa msaada kwa makundi hayo ni kuchota baraka kutoka kwa Mungu kwani hata vitabu vya dini zote ya kikristo na kiislam vinaeleza hivyo.

Ndabila alisema nguo hizo zimetolewa na waumini wa kanisa hilo kwa ajili ya kusherehekea boxing day kwa makundi hayo.

 Baadhi ya wagane na wajane waliopata msaada huo waliushukuru uongozi wa kanisa hilo kwa msaada ambao wamekuwa wakiutoa kwako hasa Askofu wa kanisa hilo, Flaston Ndabila na mke wake Janeth Ndabila.

"Kwa kweli hatuna cha kueleza zaidi ya kutoa shukurani zetu na Mungu awape afya njema na maisha marefu" alisema. Khadija Hamisi.

Mjumbe wa Serikali ya mtaa huo, Juma Hassan alisema kanisa hilo limekuwa la mfano katika kusaidia jamii ya eneo hilo kwa mambo mbalimbali na hata wakati wa mafuriko limekuwa likijitoa kurekebisha miundombinu pamoja na kuwafariji wahanga.

"Kanisa la ABC hakika ni kanisa lenye uongozi thabiti limekuwa likishirikiana na Serikali kwa mambo mengi na hata kuwanunulia madaftari na vifaa wanafunzi ambao hawana uwezo" alisema Hassan.

Alisema Askofu wa kanisa hilo Flaston Ndabila kila inapofika mwishoni mwa mwaka amekuwa akiwakumbusha kwa ajili ya kutoa misaada hiyo japo ambalo linapendeza hata mbele za Mungu.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: