Na John Walter-Babati

Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo amewahimiza vijana kuchukua mikopo kutoka Halmashauri inayotolewa bila riba ambayo inawalenga ili kujiimarisha  kiuchumi badala ya kujihusisha na maswala ya uhalifu na utumiaji wa dawa za kulevya.

Amesema kwamba Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan,  imeendelea kuwathamini Vijana, Wanawake na wenye ulemavu kwa kuwapatia mikopo hiyo ili waweze kujitegemea wenyewe na kuzirejesha fedha hizo katika Halmashauri kwa muda uliopangwa.

Sillo ametoa wito kwa vijana ambao wanakabiliwa na changamoto za kupata mikopo hiyo kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa Maendeleo ya jamii baada ya kuunda Vikundi.

Mheshimiwa Sillo aliwahimiza hayo Vijana Desemba 19, 2022 wakati anafunga ligi ya mpira wa miguu kwa vijana  kata ya Kisangaji ambapo aligawa Jezi pamoja na Mipira Kwa washindi.

Aidha Sillo aliongozana na Mwenyekiti wa Vijana (UVCCM) wilaya ya Babati Vijijini Solomoni Mpaki  ambaye aliawaasa Vijana kuendelea kusemea mazuri yote yanayofanywa na serikali ya Dr. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi wengine wa Chama walioongozana na Mbunge huyo ni katibu wa Vijana (UVCCM)  George Sanka na mjumbe wa Kamati ya utekelezaji  Nickson funga wilaya Babati vijijini.

 

Share To:

Post A Comment: