Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ameanza ukarabati wa jengo la msikiti wa Al-Masjid Salum Ally uliopo kata ya Hombolo Bwawani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake kufuatia maombi yaliyowasilishwa na waumini wa msikiti huo.


Mbunge Mavunde akiwa katika ziara zake za kawaida Hombolo Bwawani alitumia fursa hiyo jana kukabidhi vifaa vya ujenzi,madirisha ya chuma,feni na busati kwa ajili maboresho ya msikiti huo.

“Nawashukuru sana kwa heshima kubwa mliyonipa ya kuniona mimi kama naweza kuwa mdau wa kusaidia maboresho ya nyumba hii ya ibada.

Nitajitahidi kwa kadri ya uwezo wangu pamoja na marafiki zangu kufanya marekebisho makubwa ya msikiti huu kama mlivyowasilisha ombi.

Pamoja na marekebisho hayo pia nitawachangia Tsh 2,000,000 kwa ajili ya kununua ardhi ili kuongeza ukubwa wa eneo la msikiti kwa ajili ya matumizi ya vizazi vijavyo”Alisema Mavunde

Akishukuru kwa niaba ya waumini wa msikiti Al Masjid Salum Ally,Kiongozi wa Msikiti huo Mwalimu Abubakar Mohamed amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kukubali ombi lao la ukarabati wa jengo la msikiti ambao utagharimu kiasi cha Tsh 8,000,000 na kuahidi kuendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu kumjaalia kheri na baraka katika kazi zake.




Share To:

Post A Comment: