Na Denis Chambi, Tanga.
 
Joto na shauku ya kutaka kujua ninani atakuwa bingwa wa michuano ya Machupa Super Cup inayoendelea ndani ya kata ya Duga jijini Tanga linazidi kupanda timu nne zikiwa tayati zimefanikiwa kupenya katika hatua ya nusu fainali ambapo zitapepetana wikiendi hii jumamosi na jumapili kwenye uwanja wa Magomeni. 

Nusu fainali ya kwanza itashuhudiwa kandanda ikichezwa kati ya Uruguay ikiminyana na Talent FC huku ikisubiriwa kwa hamu siku ya jumapili kwenye mchezo utakaowakutanusha Jiwe FC dhidi ya Majengo FC ambapo timu mbili zitakazofuzu hatua hiyo zitakwenda kucheza fainali siku ya jumaane kumtafuta mbabe wao atakayendoka na Ng'ombe pamoja na kombe. 

Ligi hiyo imezidi kunogeshwa na mdhamini wa ligi hiyo Thomas Machupa kwani ukiachana na zawadi ambazo zitatolewa siku ya fainali tayari timu hizo nne zitakazocheza michezo yao ya nusu fainali zitavaa uzi mpya tofauti na zile ambazo walipatiwa wakati waanza hatua ya makundi jambo ambalo limezidi kuongeza ushindani wa aina yake. 

Akizungumza mratibu wa ligi hiyo Maneno Kasinge almaarufu kama Father Mau alisema kuwa michuano hiyo imekwenda vizuri kuanzia hatua ya awali hadi kufikia nusu fainali huku vikishuhudiwa vipaji na ufundi wa aina yake kutoka kwa wachezaji mbalimbali jambo ambalo litakuwa ni hazina ya baadaye kwa timu kama tu wachezaji hao watawekewa mazingira rafiki ya kimichezo. 

"Mashindano yamekwenda vizuri kuanzia ile hatua ya makundi ambayo imemalizika salama kabisa, tumeona vipaji vingi kutoka kwa wachezaji timu hizi nne zilizoingia hatua ya nusu fainali zitapata jezi seti moja moja kwajili ya hatua hiyo, vijana wana morari ya hali ya juu wanacheza mpira safi tena wa kisasa nafikiri kuna haja ya kuliyazama kundi la vijana kupitia mchezo huu wa mpira wa miguu" alisema Kasinge . 

Alisema haikuwa rahisi kwa timu hizo kufikia hatua ya nusu fainali ikizingatiwa na ushindani uliokuwepo tangu awali kila timu ikiwa inahitaji kuonyesha umwamba kwa mpinzani wake, licha ya baadhi yao kuupa lawama kwa waamuzi kwa madai ya kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu jambo ambalo linahitajika kuangaliwa kwa kina.

 " Mitizamo ya baadhi ya mashabiki kulalamikia upande wa waamuzi , ni jambo ambalo limezoeleka sasa katika kila mashindano na hata kwa upande wa ligi hii pia yametokea lakini naamini kabisha hata waamuzi wanasimamia na wanafahamu kile ambacho wanatakiwa kukifanya ila kwa sababu mashabiki wamekuwa na mapokeo tofauti na wanavyotarajia lawama kwa waamuzi ambao wanataaluma lazima ziwepo" aliongeza.

 Zawadi zipo tayari mpaka sasa kinachosubitiwa ni mshinfi tu ambapo Bingwa anaondoka na Ng’ombe na Kombe, mshindi wa pili atapata Jezi seti 1 na mipira miwili., Kipa bora, Mchezaji bora, Mfungaji bora , Kiungo bora , Kocha bora pamoja na timu yenye nidhamu.
Share To:

Post A Comment: