Na John Walter-Manyara

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wanawake viongozi kote nchini kuanzia ngazi ya kata,wilaya na hata mkoa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu agenda zinazowahusu wanawake kuhakikisha zinatekelezwa kama ilivyokusudiwa.

Aidha Dr. Gwajima ameupongeza uongozi wa Mtandao wa Jinsia nchini (TGNP) kwa kuendelea kuwa karibu na wanawake na wasichana kwa kuwapatia elimu juu ya ukatili wa kijinsia kupitia makongamano na warsha mbalimbali.

Waziri Dr. Gwajima amezungumza hayo katika Kongamano la Wanawake na Uongozi lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika kuadhimisha Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Mwenyekiti wa bodi ya TGNP Mama Gema Akilimali, amesema wapo wanaume wanaofanyiwa ukatili lakini hawatoi taarifa tofauti na wanawake ambao wapo mbele kuripoti vitendo hivyo.

Amesema katika mikakati mingi wamliyonayo nia pamoja na kupinga rushwa ya ngono ambayo TAKUKURU wanasema ni uhujumu uchumi.

“Hatutakubali sheria inayotaka kupitishwa kuwa Rushwa ya ngono inahusisha watu wote (Mwanaume na Mwanamke) tuelewe kwamba uwezekano mkubwa upo wa kumzalilisha mwanamke zaidi kuliko ile makubaliano, huenda makubaliano ni kutokana na hali halisi” alisema Akilimali

Aliendela kusema “Sasa kama TAKUKURU ilikubali kipindi kile, hatuwezi kujua kwanii wanataka kubadilisha kile kipengele kwamba wote wanahusika, tunaomba waziri uhakikishe hawabadilishili”

Amesema TGNP watahakikisha wanendelea kutoa elimu kwa wanawake na wasichana kusimama imara kukemea vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia.


Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akizungumza katika Kongamano hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam, amesema wamejikita katika kujadili,kutathmini uwekezaji wa rasilimali kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi ili kutokomeza ukatili wa kijinsia nchini.

Amesema wanawake Tanzania wapo zaidi ya asilimia 50 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 hivyo ni haki yao kupata nafasi za uongozi.

Desemba 10,2022 ni kilele cha siku ya 16 za kupinga Ukatili wa kijinsia ambapo pia itakuwa ni siku ya Haki za binadamu duniani.


Kauli mbiu mwaka 2022 "Kila Uhai una thamani,tokomeza mauaji na ukatili dhidi ya wanawake, wasichana  na watoto"

Taarifa ya mwaka 2021 inaonyesha kila siku takribani wanawake 30 wanakabiliwa na ukatili wa kijinsia.

Share To:

Post A Comment: