Jumla ya wahitimu 5,480 wamehitimu mafunzo ya kozi mbalimbali katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa mwaka wa masomo 2021/2022 ambapo kati yao wanawake ni asilimia 55.1 huku wanaume wakiwa ni asilimia 44.9.

Akizungumza katika Mahafali ya 17 yaliyofanyika katika kampasi ya Kivukoni jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Francis Michael amewataka Wahitimu wa Chuo hicho kuwa raia wema kwa kuendeleza Maadili na Uzalendo  kwa mustakabali wa Taifa

Dkt. Francis amesema hivi sasa Taifa linakabiliwa na Changamoto ya kukosekana kwa Maadili hususan kwa Vijana, hivyo amewataka Wahitimu hao kwenda kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwa wao ndiyo mabalozi sahihi katika kuelimisha na kulinda heshima ya Taifa.

Alisisitiza kuwa, dira ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ni kitovu cha utoaji Maarifa hivyo Wahitimu mnatakiwa mkayatumie vyema Maarifa mliyopata kwa kukitangaza vema Chuo.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Prof Shadrack Mwakalila alisema jukumu la Chuo ni kuendesha mafunzo ya kitaaluma,katika fani ya Sayansi jamii kwa kiwango Cha Astashahada, Stashahada, Shahada ya kwanza, shahada ya Umahiri na Shahada ya uzamivu. Kuendesha Mafunzo ya Uongozi, kufanya tafiti, Kutoa ushauri wa Kitaalaamu katika sekta ya Umma na Sekta Binafsi pamoja na kutoa huduma katika jamii.

Profesa amesema pamoja na mafanikio yaliyopatikana Chuo hapo, bado Chuo kina changamoto ya ufinyu wa bajeti katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa na Chuo katika kuboresha Mazingira ya kufundishia na kujifunzia na Upungufu wa Wanyakazi kwa mujibu wa Mahitaji Halisi ya Chuo, Jambo ambalo Serikali imeahidi kuzifanyia kazi Changamoto hizo.

Profesa Mwakalila amewapongeza Wahitimu na kuwataka kukumbuka kuwa Elimu haina mwisho, huku akiwataka Wanafunzi hao kutumia Elimu waliyoipata kuwa raia wema kwa kuendeleza Amani, Utulivu na Umoja wa Kitaifa.

Profesa amesema Mahafali haya ya 17 ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa na Wahitimu wenyewe, Wanataaluma na Wafanyakazi Waendeshaji Chini ya Uongozi wa Chuo,huku akiwataka Wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidi kwa Maslahi ya Taifa.
Share To:

Post A Comment: