Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro ameliagiz jeshi la akiba kulinda Maliasili za wilaya zikiwemo hifadhi za misitu pamoja na mazingira na kuhakikisha hakuna mtu anakata miti hovyo

Mhe. Muro ametoa maagizo hayo wakati akifunga mafunzo ya vijana 98 wa jeshi la akiba tarafa ya sepuka ambapo amesema kazi ya kulinda mazingira inapaswa kufanywa na watu waliopewa mafunzo maalum ya kupambana na wahalifu na haswa waharibifu wa mazingira ili kuliokoa taifa na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayosababishwa na uharibu wa mazingira 

Awali Akizungumza katika mafunzo hayo Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu mbali na kuwapongeza vijana hao kwa kuhitimu amewataka kuyatumia mafunzo hayo kimkakati kwa kuimarisha usalama katika kata na vijiji wanavyotoka na kuhaidi kuwapa ushirikiano wa kutosha

Dc  Muro pia amewapongeza na kuwapa zawadi wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo hayo Miongoni mwao ni Mkurugenzi wa halmashauri ya ikungi Mhe. Justice Kijazi na afisa tarafa wa sepuka Cornel Nyoni ambao sasa wanaungana na kundi la vijana 98 waliohitimu mafunzo


Share To:

Post A Comment: