Na Mario mgimba Njombe


Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement Kivegalo amemuagiza Meneja wa Ruwasa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe kuandaa mradi mkubwa wa usambazaji maji ambao utatekelezwa katika bajeti ijayo ili kutatua kero na kilio cha wananchi wa vijiji 18 vilivyopo mwambao wa Ziwa Nyasa. 


Katika ziara ya kikazi ya Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa Mhandis Kivegalo ambayo ameifanya hiyo kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na serikali  fedha zaidi ya shilingi bilioni 7.4 kwenda kutatua changamoto ya ukosefu wa maji kwa wananchi ambao  hawajawahi kupata ya maji ya bomba safi na salama tangu vianzishwe.


Akisoma taarifa  Meneja wa Ruwasa wilaya ya Ludewa, Mhandisi Mlenge Katulilo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa amekiri kuwa vijiji 17 vilivyopo mwambao wa ziwa Nyasa havijawi kupata maji safi na salama.


Aidha Kutokana hali hilo Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa Mhandis KIvegalo alitoa maelekezo kwa Meneja wa Ruwasa wilaya ya Ludewa akiwa katika eneo la Mradi wa ujenzi wa matenki ya maji yaliyopo Kata ya Ludewa mjini yaliyofikia asilimia 15 


Monika Mchilo Diwani wa Kata ya Ludewa Mjini alisema kuwepo kwa utekelezaji wa mradi huu utatusaidia wananchi kutatua changamoto hiyo ambayo likuwa ikuwakabili wananchi ya kukosekana kwa maji safi na salama na kufikiwa kwa mradi huo utaouguza changamoto hiyo.


Imeelezwa kukamilika kwa ujenzi wa matenki makubwa mawili ya mradi wa usambazaji maji katika kata ya Ludewa mjini unatarajiwa kuwahudumia wananchi zaidi ya elfu 15 hali ambayo baadhi ya wananchi wameishukuru serikali.

Share To:

Post A Comment: