Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.Selemani Jafo akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Bi Anne Veathe Tvinnereim katika banda la maonesho la Tanzania Sharm El-Sheikh, Misri. Mawaziri hao wametoa tamko la pamoja la kushirikiana katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani
Jafo leo tarehe 9 Novemba 2022 katika vikao vya pembezoni mwa Mkutano wa Nchi
Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi jijini
Sharm El Sheikh nchini Misri, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa
Mambo ya Nje na Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Bi Anne Veathe Tvinnereim
katika banda la maonesho la Tanzania.

Katika mazungumzo hayo, mawaziri hao wamejadili na kukubaliana kuendeleza
ushirikiano katika masuala ya maendeleo na hususan ufadhili katika miradi ya
hifadhi ya mazingira na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Jafo amesema Serikali ya Tanzania na Norway zimekuwa na ushirikiano wa
muda mrefu katika sekta mbalimbali na kusisitiza kuwa kwa sasa masuala ya
mazingira yanazidi kupewa kipaumbe katika ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Bi. Anne Veathe
Tvinnereim amesisitiza kuwa nchi ya Norway itaendelea kushirikiana na kufadhili
miradi ya mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania kwa lengo la kusaidia wananchi
walio katika hatari kubwa ya kuathiriwa na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Waziri Jafo alimshukuru Bi Anne Veathe Tvinnereim na Serikali
ya Norway kwa ujumla kwa ushirikiano na misaada katika sekta mbalimbali za
kiuchumi kwa Tanzania.

 Alisema Tanzania iko tayari kushirikiana na Serikali ya
Norway na kuendeleza ushirikiano huo kwa maslahi mapana ya nchi na maendeleo
ya Taifa kwa ujumla. Alisisitiza kuwa ajenda ya mabadiliko ya tabianchi ni
changamoto kubwa duniani na inahitaji ushirikiano na ufadhili wa nchi zilizoendelea
na zinazoendelea.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.Selemani Jafo akimkabidhi nyaraka mbalimbali Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo ya Kimataifa wa Norway Bi Anne Veathe Tvinnereim katika banda la maonesho la Tanzania Sharm El-Sheikh, Misri leo tarehe 09/11/2022, mara baada ya kukamika kwa mazungumzo ya ushirikino baina yao.

Share To:

Post A Comment: