MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau juu ya kuanzishwa kwa mfuko wa Maji Tanga uliofanyika mjini kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo na kushoto ni  Afisa Mazingioa Mkoa wa Tanga Thimosi Sosia.

Na Oscar Assenga,TANGA.

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amesema iwapo haku takuwa na uwekezaji mzuri kwenye vyanzo vya maji kuna uwezekano mkubwa kwa siku zijazo kukosekana kwa huduma hiyo muhimu kwa jamii.

Mgandilwa aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau juu ya kuanzishwa kwa mfuko wa Maji Tanga uliofanyika mjini hapa ambapo alisema hivyo kupitia elimu hiyo ni vema wakarudi kwenye taasisi zao wakashauri namna ya kuwekeza kwenye vyanzo vya maji.

Mkuu huyo wa wilaya alisema hivyo ni muhimu kwa wenye viwanda na wawekezaji wakaona namna nzuri ya kutumia sehemu ya faida zao kwa ajili ya kuwekeza kwenye miradi ya maji iwe kuchangia moja kwa moja katika mfuko au kuwekeza kwenye utunzaji wa vyanzo vya maji.

Alisema kwasababu hakuna kiwanda bila rasilimali maji hivyo kila mmoja kwenye kampuni yake na taasisi yake kila anachokifanya kina umuhimu mkubwa sana kwenye maji hivyo wawekeze kwenye vyanzo vya maji ili kuisaidia jamii.

"Naombeni mkitoka hapa muone namna ya kwenda kujenga uelewa namna ya kutunza vyanzo vya maji kwa lengo la kuviwezesha viwe endelevu kwa ajili ya vizazi vya sasa na baadae pamoja na kuona namna gani mnaweza kushiriki katika uwekezaji wa miradi ya maji" Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kwamba hivi sasa kuna changamoto mbalimbali hasa ya ya ulimaji usio endelevu pamoja na ufugaji wa mifugo holela na utiririshaji wa maji machafu kwenye vyanzo vya maji jambo ambalo linaathari hivyo ni vema Jamii ikabadilika na kuachana navyo.

"Lakini changamoto nyengine ni wananchi bado wana tabia ya kuoga na kufua kwenye vyanzo vya maji hayo yote yanatokea ni msingi mkubwa watanzania walio wengi hivi sasa tumekuwa wabinafsi tofauti na zamani tunaangalia maslahi yetu binafsi kuliko kutazama ile halaiki na ujumla"Alisema.

Hata hivyo alisema kupitia umoja wao waweke mikakati namna gani wanaweza kukabiliana na uharibifu wa hivyo vyanzo ili viendelee kuwa endelevu kwa maisha ya sasa na baadae

"Hivyo nisisitize suala la uhifadhi wa vyanzo vya maji ni mtambuka sasa kwani watanzania wengi wanaona suala la utunzaji wa maji sio wajibu wetu bali ni wajibu wa Mamlaka husika hii sio sawa lazima tushirikiane kutunza na kuvilinda" Alisema.

Hata hivyo Mkuu huyo.wa wilaya alisema kwa namna dunia inavyokwenda miaka michache mbele ya safari rasilimali maji itakuwa mtihani sana na itakuwa na thamani kubwa kwamba mtu yoyote ambaye anatumia maji lazima awe ni mtu mwenye nafasi hiyo.

Alisema kupitia kikao hicho ni wajibu wa kila mwananchi kuona anasababu ya kutunza vyanzo vya maji ili hiyo rasilimali iwe inatumika vizuri ili iweze kuwa endelevu.

Awali akizungumza wakati wa mkutano huo Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo alisema kuwa mfuko utaweza kuongeza nguvu katika jitihada walizozianzisha za utunzaji wa vyanzo vya maji kwa kuwapatia shughuli mbadala wananchi wanaoishi kando ya vyanzo hivyo.

Alisema kuwa shughuli za utunzaji wa vyanzo vya maji inahitaji uwekezaji mkubwa ushiriki wa wadau utaweza kutoa matokeo changa na hivyo kusaidia katika kumaliza changamoto ya uharibifu iliyopo.

MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau juu ya kuanzishwa kwa mfuko wa Maji Tanga uliofanyika mjini kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo na kushoto ni Afisa Mazingioa Mkoa wa tanga Timosi Sosia
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa na kushoto ni Afisa Mazingira Mkoa wa Tanga Thimosi Sosia
MKURUGENZI wa Bodi la Maji la Mto Pangani Segule Segule akizungumza 
Afisa Mazingira Mkoa wa Tanga Thimosi Sosia akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo
MKUU wa wilaya ya Pangani Ghalib Ringo akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo Mwalimu Hassani Nyange na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulidi Surumbu na wa kwanza kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga Joseph Sura






Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: