DENIS CHAMBI, TANGA 

TAASISI ya maendeleo ya jamii Tengeru iliyopo mkoani Arusha imepanga kukutana na wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama wamachinga waliopo ndani ya jiji la Tanga lengo hasa likiwa ni kuwapa elimu ya namna bora ya kuhudumia wateja na kupata mikopo itakayomsaidia kumuongezea mtaji katika biashara yake. 

Hayo yameelezwa na mratibu wa michezo kutoka katika taasisi hiyo Elifadhili Mpehongwa wakati walipowasili mkoani Tanga kwaajili ya kushiriki mashindano ya shirikisho la michezo inayojumuisha Taasisi mashirika na makampuni binafsi maarufu kama SHIMUTA kwa mwaka huu wa 2022 ambapo wamejitamba kuwa watahakikisha hawarudi mikono mitupu Arusha badala yake kuweka kuipa heshima taasisi hiyo kupitia michezo watakayoshiriki.

 "Pamoja na michezo hii ya SHIMUTA tuna kazi ambayo tutaifanya katika jiji hili la Tanga ya kukutana na kutoa elimu kwa wamachinga katika maswala ya huduma kwa wateja lakini pia namna ambavyo mtu anaweza akapata mkopo katika vikundi na benki mbalimbali" alisema Mpehongwa

 "Tunawaahidi wanafunzi na watumishi wa chuo chetu kwamba mwaka huu tutampiga mtu kipigo ambacho ni cha mpira maendeleo tutafanya michezo katika weledi mkubwa na watu watajionea kwamba taasisi yetu imeendelea katika kipengele cha michezo" alisema.

 Akizungumzia maandaliziyao katika michezo kwa timu zao kocha Omati Mwingira amesema kuwa wamejipanga vilivyo katika kuhakikisha kwamba kila mchezo unakuwa ni fainali kwao huku wakitambua ushindani baina yao na timu watakazokutana nazo jambo ambalo wanaamini haitakuwa rahisi. 

"Tumefanya maandalizi ya kucheza mechi nyingi tumetoka Arusha tukiwa tunaongoza ukanda wetu wa Kaskazini na kwenye SHIMUTA hii kuna jambo tumelileta hapa Tanga" 

"Najua watu wa chuo cha Tengeru wapo nyuma yetu ila kikubwa walichotutuma kuleta Tanga hapa ni kucheza soka la maendelwo na soka safi na kupata ushindi kikubwa tumefwata kombe watusubirie kwa hamu naamini tutamaliza salama na kufanikiwa kuondoka na Kikombe na kuzitaka timu pinzani watakazokutana nazo kujipanga kweli kweli " alisema 

Mashindano hayo yatashirikisha michezo ya mpira wa miguu kwa wanaume, mpira wa Pete , Wavu, Kikapu, Dats, Pool table, Vishale , Draft kukimbia kwa magunia, Riadha kuvuta kamba Bao na mingineyo kedekede, lengo kuu hasa ikiwa ni kuimarisha mahusiano baina ya taasisi, mashirika na makampuni kuimarisha afya kupitia michezo ikiwa pia ni kuondokana na magonjwa yasiyoambukiza. 

Michezo hiyo ambayo hufanika kila mwaka ni kwa mara ya pili mfululizo kufanyika ndani ya mkoa wa Tanga mwaka huu yakija na kauli mbiu ya 'SHIMUTA familiya moja'
Share To:

Post A Comment: