Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Serikali inakamilisha  tathmini  ya upembuzi yakinifu wa shule zote za Msingi  kupitia mradi wa kuboresha elimu ya awali na msingi Tanzania Bara (BOOST) ili kuandaa mpango endelevu wa uboreshaji wa elimu ya awali na msingi nchini .

Hayo yamesemwa leo Novemba 1, 2022 na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Davidi Silinde kwenye Mkutano wa Tisa wa Bunge, kikao cha kwanza kilichofanyika Jijini Dodoma 

Akijibu swali la Mhe. Joseph Kakunda Mbunge wa Sikonge aliyetaka kujua lini srikali itajenga shuke mpya ya msingi katika maeneo ya Mbirani,Makibo, Kiyombo na Tutuo Mhe. Silinde amesema serikali imeamaua kufanya tathmini hiyo kwa lengo la kubaini taarifa za eneo la shule ilipo, hali ya mazingira ya shule, umbali wa shule moja hadi nyingine  na umbali wa shule na makazi ya watu  ili kandaa mpango endelevu wa uboreshaji  elimu nchini

Amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 kupitia mradi wa Boost Serikali imetenga Shilingi bilioni 230 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi katika Halmashauri zote 184 ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.

Share To:

Post A Comment: