Wakazi wa kijiji cha Lole kata ya Ikuna wilayani Njombe wamesema wangali wanataabika kupata huduma za matibabu umbali mrefu kutokana na kukosa zahanati jambo linalowapa wakati mgumu na kutumia gharama kubwa pindi wanapokwenda Ikuna kutibiwa.

Mratibu wa mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF Halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Steward Vidoga amefika kijijini hapo kuzindua mradi wa ujenzi wa nyumba ya wataalam wa afya baada ya zahanati kujengwa ambaye anatumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuonesha ushirikiano katika ujenzi huo ili mwakani zahanati ianze kufanyakazi.

Wakizungumza kijijini hapo baada ya serikali kupitia mradi wa TASAF kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa zahanati pamoja na nyumba ya watumishi wa afya itakayogharimu milioni 66 wananchi hao wanasema sasa huenda wakapunguziwa adha hiyo baada ya ujenzi kukamilika.

Lukas Kihombo,Augustino Sambanaye na Theudora Mbuna ni wakazi wa kijiji cha Lole ambao wanakiri kuwa adha ambazo wamekuwa wakizipata wakati wa kutafuta huduma za afya zitakwenda kukoma kwa kupata mradi wa zahanati hiyo pamoja na nyumba ya wauguzi.

Baadhi ya viongozi wa kamati ya ujenzi wa zahanati na Nyumba hiyo katika kijiji cha Lole akiwemo Eliza Jonas na Bryson Ngimbudzi wamewataka wananchi na viongozi wengine kuonesha mashirikiano ili kukamilisha ujenzi huo.

Vijiji vya Lole na Ikando vimepatiwa kiasi cha shilingi milioni 92 kila kijiji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ambazo tayari zimejengwa na zinasubiri vifaa na watumishi huku zahanati ya Lole ikipata na fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya waganga.


Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: