Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Juma Mkomi (katikati) akisisitiza Jambo kuhusu ukarabati wa Miundombinu ya Barabara ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro


 Na Kassim Nyaki, NCAA


Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma Mkomi ameielekeza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutunza mitambo iliyonunuliwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara zilizoko ndani ya hifadhi ambayo ilinunuliwa kupitia fedha za mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Bw. Mkomi ametoa maelekezo hayo tarehe 19 Novemba, 2022 wakati wa ziara aliyoifanya katika Hifadhi ya Ngorongoro yenye lengo la kukagua miundomibu ya barabaraba iliyojengwa kupitia fedha za UVIKO ambapo Serikali iliipatia NCAA shilingi bilioni 6.6 kwa ajili ya ununuzi wa mitambo ya barabaraa na kazi uboreshaji wa miundombinu ndani ya Hifadhi.

Naibu Katibu Mkuu ameupongeza uongozi wa NCAA kwa usimamizi mzuri wa ukarabati wa barabara ndani ya hifadhi na kusisitiza kuwa jitihada za ukarabati ziendelee kufanyika mara kwa mara ili barabara ziwe bora na kusaidia huduma kwa watalii hasa kuelekea mwisho wa mwaka ambapo idadi ya wageni na magari huongezeka katika maeneo ya vuvutio vya utalii vilivyopo katika hifadhi hiyo.

Naibu Kamishna wa NCAA (Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii) Dkt. Christopher Timbuka amemueleza Naibu katibu Mkuu huyo kuwa NCAA kupitia fedha za mradi huo imekarabati barabara zenye urefu wa kilomita 80 zinazojumuisha njia kuu ya kutoka eneo la Seneto hadi golini yenye urefu wa kilomita 55, barabara ya kutoka makumbusho ya Olduvai hadi Jabali la Nasera yenye urefu wa kilomita 25 na kipande cha Kilomita 5 kinachounganisha barabara kuu ya Seneto- Golini kuelekea Makumbusho ya olduvai.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa UVIKO kutoka NCAA Kamishna Msaidizi Mwandamizi Dkt. Johnson Saiteu Laizer ameeleza kuwa, mbali na ukarabati wa kilomita 80 ndani ya Hifadhi, kupitia fedha hizo NCAA imenunua seti ya mitambo ya ujenzi wa barabara zilizoko ndani ya hifadhi.

Amebainisha kuwa kati ya seti iliyoagizwa tayari mitambo 3 inayojumuisha Greda moja, mtambo wa kushindilia, mtambo wa kuchimbia na pickup mbili zimeshapokelewa na zinafanya kazi, aidha malori mengine manne na boza moja la maji vinatarajiwa kupokelea kabla ya mwisho wa mwaka.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Juma Mkomi (Kulia) akishuhudia mtambo wa kushindilia barabara katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro
Sehemu ya Barabara ya Kutoka Seneto hadi Golini iliyokarabatiwa kupitia fedha za UVIKO-19
Mratibu wa Mradi wa UVIKO NCAA Kamishna Msaidizi Mwandamizi Dkt. Johnson Saiteu Laizer akitoa taarifa ya utekelezaji wa fedha za Mradi wa UVIKO-19 katika Hifadhi ya Ngorongoro

 Naibu Kamishna wa NCAA Dkt. Christopher Timbuka (katikati) akielezea uboreshaji wa Barabara ya kutoka Makumbusho ya Olduvai hadi Jabali la Nasera yenye urefu wa kilomita 25 wakati wa ziara ya Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Share To:

Post A Comment: